SHULE YA DON BOSCO YAHITIMISHA WIKI YA MICHEZO,DC MTATIRO AIPONGEZA KUIBUA NA KUKUZA VIPAJI VYA WANAFUNZI
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro, ameipongeza Shule ya Sekondari Don Bosco iliyopo Didia wilayani Shinyanga, kwa kuendeleza utamaduni wa michezo shuleni hapo,jambo ambalo linasaidia kuibua na kukuza vipaji vya wanafunzi,na kuimarisha afya zao.
Mtatiro amebainisha hayo leo, Machi 8, 2025, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika uhitimishaji wa wiki ya michezo ya Don Bosco,akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha.
Akizungumza katika bonanza hilo,Mtatiro amesema michezo kwa wanafunzi ni muhimu kwa kuimarisha afya zao, kuibua vipaji,kuwajengea nidhamu,kupumzisha akili zao, na hata kufanya vizuri kitaaluma.
Aliongeza kuwa michezo ni sehemu muhimu ya maisha ya kila mtu, na wataalamu wa afya wanasisitiza umuhimu wa kufanya mazoezi ili kuepukana na magonjwa nyemelezi.
“Hili jambo la michezo hapa DonBosco nimelipenda. Utamaduni huu ni mzuri sana, natamani hata kwa shule za serikali tuanzishe mashindano kama haya ili kusaidia kuimarisha afya za wanafunzi, kuibua vipaji,kupumzisha akili zao na kujenga nidhamu,”amesema Mtatiro.
Pia,ametoa nasaha kwa wanafunzi, akiwashauri waendelee kushiriki michezo, kuwa na nidhamu, na kupenda masomo ili waweze kutimiza ndoto zao na kuwa viongozi bora wa baadaye katika taifa hili.
Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari Don Bosco, Padri Amani Meela, amesema kuwa shule hiyo inatambua umuhimu wa michezo, na kwamba michezo shuleni hapo ni sehemu ya malezi ya watoto, na inajenga nidhamu, kukuza ufanisi wa kitaaluma,kuboresha afya, na kuibua vipaji.
Padri Meela amefafanua kuwa wiki hiyo ya michezo ilianza Machi 1, 2025, na imehitimishwa leo Machi 8, kwa michezo mbalimbali ikiwamo riadha, mbio za baiskeli, kuvuta kamba, sarakasi, pamoja na kuonyesha vipaji mbalimbali kupitia "houses" za shule, huku washindi wakipewa zawadi na vikombe vya ushindi.
Kaka Mkuu wa shule hiyo Meshack Hunge,amesema michezo hiyo kwao inawajenga kiafya,kiakiri,kuibua vipaji vyao,kuimarisha udugu, sababu katika michezo hiyo hua wanaalika na shule za jirani kushiriki nao na kufurahi pamoja.
TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza.
Mkuu wa shule ya DonBosco Padri Amani Meela akizungumza.
Mkurugenzi wa Shule ya DonBosco Padri Nicodemas Orioki akizungumza.
Kaka Mkuu wa shule ya DonBosc Meshack Hunge akisoma Risala ya wanafunzi.
0 Comments