6/recent/ticker-posts

RPC SHINYANGA KAMANDA MAGOMI AONYA WATAKAOVURUGA AMANI KABLA NA WAKATI WA UCHAGUZI,MADEREVA BODABODA NA BAJAJI WAMPONGEZA KWA ELIMU


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi,akizungumza na waendesha bajaji na bodaboda Manispaa ya Shinyanga.

Chanzo Shinyanga Press club Blog

JESHI la Polisi mkoani Shinyanga limewahakikishia wananchi wa mkoa wa Shinyanga na kuonya watu wenye nia ya kuvuruga amani na utulivu kabla na wakati wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025, na kuwataka wajitokeze kwa wingi kutumia haki yao ya kikatiba kwa kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka kwani jeshi la polisi limejipanga vizuri kuhakikisha ulinzi na usalama unaimalika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi, ametoa kauli hiyo leo Oktoba 18, 2025, wakati akizungumza na waendesha bajaji ,bodaboda na magari madogo (haice) katika stend ndogo ya Soko Kuu la mjini Shinyanga.

Magomi amesema kuwa Jeshi hilo lipo kamili kulinda Amani siku ya Uchaguzi Mkuu, na kwamba wananchi wasiwe na wasiwasi, bali wajitokeze kwa wingi kupiga kura, na kutumia haki yao ya kikatiba kuwachagua viongozi wanaowataka ambao watawaongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.


“Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga tumejipanga vyema kuhakikisha amani inaendelea kutawala siku zote na siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29,tunawaomba wananchi wote wajitokeze kwenda kupiga kura sababu amani itakuwepo na hakutakuwa na vurugu zozote,”amesema Magomi.

Aidha kamanda Magomi amewaonya watu au baadhi ya vikundi ambavyo vimepanga kufanya vurugu siku ya uchaguzi, kwamba wasije kuthubutu, kwa kuwa jeshi la polisi limejipanga vyema kudhibiti fujo huku akisisitiza kuwa jeshi hilo halitasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya mtu au kikundfi chochote kitakacho jaribu kuvuruga amani.


Naye Mwenyekiti wa Boda Boda Manispaa ya Shinyanga Juma Mrabu, amesema vijana wa bodaboda hawapo tayari kutumika kuvuruga amani ya nchi siku ya Uchaguzi Mkuu,bali watashiriki kwenda kupiga kura na kurudi kuendelea na shughuli zao kama kawaida za kujitafutia kipato.

Oktoba 29 ni siku ya kupiga kura ya kuchagua Rais,Wabunge na Madiwani ambao wataongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo hadi 2030.

TAZAMA PICHA👇👇

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi akizungumza .








Post a Comment

0 Comments