Benki ya NMB Kanda ya Magharibi imeng'ara katika mchezo wa kirafiki baada ya kuibuka kidedea kwa kuifunga timu ya CRDB Al Barakah Kanda ya Magharibi magoli 4 kwa 2 katika mchezo wake wa kirafiki uliopigwa hii leo katika uwanja wa Shule ya Sekondari Tabora mkoani Tabora .
Awali akizungumza na Wachezaji wa Timu zote mbili Bw.Urio amesema kuwa lengo la mchezo huo nikudumisha umoja na mshikamano baina ya Timu hiyo huku akiahidi kuendeleza utaratibu huo wakuandaa michezo ya kirafiki baina ya Taasisi mbali mbali kwa kuamini kuwa Michezo ni furaha ,Michezo ni afya,Michezo udumisha umoja na mshikamano baina ya Taasisi na Taasisi.
Kwa upande wake meneja watimu ya Timu ya CRDB Al Barakah Kanda ya Magharibi Gabriel Hatibu amekiri kufungwa na benki ya NMB Kanda ya Magharibi huku akipongeza ushirikiano ulio onyeshwa na Uongozi wa benki ya NMB Kanda ya Magharibi kwa kuandaa mchezo huo ambao umewakutanisha na kutoa burudani yenye mvuto kwa wapenzi wasoka mkoani Tabora,Nakuahidi kujipanga kwa michezo kwa kukinoa kikosi cha CRDB kwa ajili ya Michezo mingine.
TAZAMA PICHA ZOTE HAPA CHINI.
0 Comments