6/recent/ticker-posts

MASHINDANO YA KATAMBI UNDER 17 CUP HATUA YA NUSUFAINALI YA ENDELEA KUTOA TABASAMU KWA MASHABIKI ,BUSULWA SEC YA TINGA FAINALI

Na Mwandishi wetu Amoj Media Shinyanga.

Mashindano ya mpira wa miguu yanayojulikana kama SHIDIFA Under 17 League, maarufu kama Katambi Under 17 Cup 2025, yameendelea kutimua vumbi katika uwanja wa Shule ya sekondari Busulwa ikiwa ni hatua ya nusu fainali kwa kuzikutanisha timu ya Ngokolo Sekondari dhidi ya timu ya Busulwa Sekondari ambapo mpambano huo umemalizika kwa timu ya Busulwa sekondari kuibuka kidedea kwa kuifunga timu ya Ngokolo sekondari Mabao mawili kwa sifuri na kupata tiketi ya kutinga fainali.

Mashindano hayo yaliyo anza kutimua vumbi Februari 14, 2025,yakishirikisha timu 16 yanaendelea katika hatua ya nusu fainali kwa udhamini wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

Mashindano haya, ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya michezo kwa vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 17, yanatarajiwa kuwa jukwaa la kuibua vipaji vya vijana wa mtaa na wanafunzi wa shule za sekondari.

Katika mashindano hayo Mhe.Katambi ametoa fedha kiasi cha shilingi milioni 6,610,000/- kwa Kamati tendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Shinyanga (SHIDIFA) ikiongozwa na mwenyekiti wake Joseph Assey ikiwa ni dhamira  ya dhati ya Mbunge huyo kusaidia maendeleo ya michezo katika jimbo la Shinyanga mjini.

Akizungumza na wanamichezo pamoja na mamia ya mashabiki walio fika uwanjani kutazama mpambano huo Katibu wa 
Mbunge Samwel Jackson, ameeleza umuhimu wa michezo kwa vijana kuwa nipamoja na kuimarisha afya za vijana pamoja na kuwapatia ajira vijana wenye vipaji huku akiomba wadau wamichezo kuendelea kujitokeza katika viwanja mbalimbali ili waweze kuchagua vijana wenye vipaji na kuwaendeleza.

Kwa upande wake Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wawilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro baada ya kutazama nusufainali hiyo amempongeza Mhe.Katambi kwa moyo wake wakujitoa kuendeleza vipaji vya vijana wa jimbo la Shinyanga mjini na kuwaomba wadau wengine kuiga mfano huo.
Vicheko na tabasamu vikiendelea kwa watazamaji wa Mashindano ya Katambi Under 17 Cup 2025,hatua ya nusufainali ya kwanza katika viwanja wa Busulwa sekondari.
Shangwe zikiendelea kwa mashabiki wa shule ya sekondaro Busulwa Mashindano ya Katambi Under 17 Cup 2025,hatua ya nusufainali ya kwanza katika viwanja wa Busulwa sekondari.

Mashindano ya Katambi Under 17 Cup 2025,hatua ya nusufainali ya kwanza katika viwanja wa Busulwa sekondari ya kiendelea.Mashindano ya Katambi Under 17 Cup 2025,hatua ya nusufainali ya kwanza katika viwanja wa Busulwa sekondari ya kiendelea.

Shangwe zikiendelea kwa mashabiki wa shule ya sekondaro Busulwa Mashindano ya Katambi Under 17 Cup 2025,hatua ya nusufainali ya kwanza katika viwanja wa Busulwa sekondari.

Shangwe zikiendelea kwa mashabiki wa shule ya sekondaro Busulwa Mashindano ya Katambi Under 17 Cup 2025,hatua ya nusufainali ya kwanza katika viwanja wa Busulwa sekondari.

Watazamaji wa Mashindano ya Katambi Under 17 Cup 2025,hatua ya nusufainali ya kwanza katika viwanja wa Busulwa sekondari wakiendelea kutazama burudani.

Wachezaji wakijinadaa na mchezo wa Mashindano ya Katambi Under 17 Cup 2025,hatua ya nusufainali ya kwanza katika viwanja wa Busulwa sekondari .
Watazamaji wa Mashindano ya Katambi Under 17 Cup 2025,hatua ya nusufainali ya kwanza katika viwanja wa Busulwa sekondari wakiendelea kutazama burudani.
Shangwe zikiendelea kwa mashabiki wa shule ya sekondaro Busulwa Mashindano ya Katambi Under 17 Cup 2025,hatua ya nusufainali ya kwanza katika viwanja wa Busulwa sekondari.

Post a Comment

0 Comments