6/recent/ticker-posts

RC MACHA AONGOZA SHEREHE YA UTOAJI TUZO KWA WALIPA KODI BORA WA MKOA WA KODI KAHAMA NA SHINYANGA ,AONYA WAKWEPAJI KODI

Mhe.mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza na wadau wakodi na kuwasisitiza juu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari kabla ya kuanza zoezi la kukabidhi tuzo.

Na Amo Blog Shinyanga.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kikodi Shinyanga na Kahama, jana Februari 28,2025, wamefanya sherehe maalum ya utoaji tuzo kwa Walipakodi waliofanya vizuri zaidi katika mwaka wa fedha 2023/24. Sherehe hii ni sehemu ya juhudi za TRA kuwatambua na kuwapongeza walipakodi hao kwa mchango wao mkubwa katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha mapato ya taifa yanaongezeka kupitia ulipaji wa kodi.

Sherehe hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Malex Hotel, uliopo Wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali, wakiwemo viongozi wa TRA, wawakilishi kutoka ofisi za serikali, na watoa huduma mbalimbali,lengo kuu la sherehe hii likiwa ni kutoa motisha na hamasa kwa walipakodi bora ili kuongeza tija katika ulipaji wa kodi, kwani mchango wao ni muhimu kwa maendeleo ya taifa.

Katika hotuba yake, mgeni rasmi ambye ni mhe.mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha amesisitiza umuhimu wa wafanya biashara kulipa kodi kama sehemu ya kutimiza wajibu wao,nakuwapongeza walipakodi kwa umahiri wao katika kutimiza majukumu yao ya kulipa kodi kwa wakati hali inayo saidia kuchochea maendeleo yanchi kwa kutekeleza miradi ya maendeleo. 

Aidha Mhe.Macha  amesema kuwa sherehe hizi si tu kwa kutambua mafanikio ya walipakodi, bali pia ni sehemu ya kuhamasisha jamii ya wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa wakati na kwa uwazi.

Kwa upande wao baadhi ya  walipakodi walioshinda tuzo hizo, wamekiri kuwa ufanisi wao umetokana na juhudi za kufuata sheria na kanuni za kodi, pamoja na ushirikiano mzuri wanao upata kutoka TRA huku Wakielezea furaha yao kwa kutambuliwa na kupewa tuzo, na kuahidi kuendelea kutoa mchango wao katika kulipa kodi kwa manufaa ya taifa.

Sherehe hiyo ilikuwa ni fursa ya kuonyesha mfano mzuri wa uwajibikaji katika ulipaji kodi na imejenga hali ya ushirikiano zaidi kati ya TRA na walipakodi, jambo ambalo ni muhimu katika kufikia malengo ya taifa ya kukuza uchumi na maendeleo endelevu.Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania mkoa wa Shinyanga Emmanweli Maro akimkabidhi tuzo Mhe.mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha kwa ushirikiano anao utoa kwa TRARAMhe.mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akimkabidhi tuzo mkurugenzi wa ubunifu na chapa ya matangazo kutoka kampuni ya jambo Groop ambaye na Jambo media Nickson George

Mhe.mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akimkabidhi tuzo mkurugenzi wa ubunifu na chapa ya matangazo kutoka kampuni ya jambo Groop ambaye na Jambo media Nickson George

Mhe.mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akiendelea na zoezi la kukabidhi tuzo kwa washindi.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania mkoa wa Shinyanga Emmanweli Maro akiendelea na zoezi la kukabidhi tuzo kwa washindi.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa kodi Kahama Warioba Kanire akikabidhi tuzo kwa washindi.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa kodi Kahama Warioba Kanire akikabidhi tuzo kwa washindi.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa kodi Kahama Warioba Kanire akimkabidhi tuzo Mhe.Mkuu wawilaya ya Kahama Mboni Mhita kwa ushirikiano mzuri anao toa kwa TRA.
Mhe.Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita akiendelea na zoezi la kabidhi tuzo kwa washindi 
Mhe.Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita akiendelea na zoezi la kabidhi tuzo kwa washindi 
Mhe.Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita akiendelea na zoezi la kabidhi tuzo kwa washindi 
Mwakilishi wa kamishina mkuu wa mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Emmanwel Nko akiendelea na Zoezi la kukabidhi tuzo kwa washindi 

Katibu tawala wilaya ya Kahama Glory Abisalum akiendelea na zoezi la kukabidhi tuzo kwa washindi .

Wadau wa tuzo wakiendelea kufatilia zoezi la utoaji wa tuzo kwa washindi.
Wadau wa tuzo wakiendelea kufatilia zoezi la utoaji wa tuzo kwa washindi.
Mc Amos John (MC Mzungu mweusi akimkaribisha mgeni rasmi mhe.Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha kwa ajili ya zoezi la utoaji wa tuzo kwa washindi.

Tazama picha zote za matukio na Imani Grapher Kahma

Post a Comment

0 Comments