

Leo,
April 6, 2025, uongozi wa Taasisi ya Nasimama na Mama Popote Nilipo Mkoa
wa Shinyanga ukiongozwa na mwenyekiti wa taasisi hiyo mkoa wa Shinyanga Bi.Zamda Shabani pamoja na katibu wa Taasisi Bi.Tatu Almas umefanya kikao cha kipekee kilichofanyika katika eneo la Mazingira
Senta, Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la viongozi wamkoa kutaka kufahamiana na
kupanga mikakati ya kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kupata ushindi mkubwa
katika uchaguzi mkuu ujao.
Viongozi wa taasisi hiyo wametumia
fursa hiyo kumpongeza Rais Samia kwa uongozi wake imara na juhudi zake za
kuleta maendeleo nchini.
Katika mkutano huo, viongozi wa
taasisi hiyo wameelezea jinsi Rais Samia alivyokuwa na mchango mkubwa katika
kuboresha sekta mbalimbali za kiuchumi, kijamii, na kisiasa, huku wakisisitiza
kuwa ni muhimu kumuunga mkono ili kuendeleza mafanikio hayo.
Aidha viongozi hao wamebainisha kuwa Rais
Samia ni kiongozi ambaye ameonyesha uwezo wa kuleta mabadiliko na maendeleo
endelevu, hivyo wanajukumu la kuhakikisha anapata sapoti kubwa kutoka kwa
wananchi, hasa katika mkoa wa Shinyanga katika kipindi hiki cha kuelekea
uchaguzi mkuu.
Katika kikao hicho, viongozi wa
taasisi ya Nasimama na Mama wamejadili na kupanga mikakati ya kuhamasisha
wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Samia, ikiwa ni sehemu ya jitihada za
kuhakikisha anapata ushindi mkubwa.
Pia Mwenyekiti wa Taasisi ya Nasimama na Mama Popote
Nilipo Kanda ya Serengeti, Osca Kaijage, pamoja na Katibu wa Kanda
ya Serengeti, Bw. Renatus Nzemo, wamehudhuria kikao hicho na kutoa michango muhimu.
Kaijage amesisitiza umuhimu wa viongozi wa
taasisi kushirikiana kwa karibu na jamii, na kumsaidia Rais Samia kupata
ushindi kwa kishindo katika uchaguzi mkuuu
Pamoja na kujadili masuala ya
kisiasa, kikao hicho pia kimejadili masuala ya kijamii, hasa mapambano dhidi ya
ukatili ambapo Wanachama wa taasisi wameonyesha dhamira ya kushirikiana na
wadau mbalimbali katika kupambana na ukatili, kwa lengo la kuhakikisha kuwa
jamii inakuwa na usalama na ustawi iwapo wataungana kukemea vitendo vya
ukatili, hasa kwa wanawake na watoto.
Katika mjadala huo, wameeleza kuwa ni
muhimu kuwafikia watu wengi kwa kutoa elimu ya madhara ya ukatili na jinsi ya
kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji.
Katika kumalizia kikao hicho,
wanachama wa taasisi wameeleza dhamira yao ya kuendelea kushirikiana na
Serikali ya Rais Samia katika kutokomeza vitendo vya ukatili na kuhakikisha
kuwa jamii inakuwa na mazingira salama huku wakisisitiza kuwa ni muhimu kuwa na
mfumo imara wa kutoa msaada kwa wahanga wa ukatili, pamoja na kuongeza
uhamasishaji kwa jamii kuhusu umuhimu wa haki na usawa kwa wote.
Kwa
kumalizia, wanachama wa taasisi hiyo walionesha wazi kuwa wataendelea
kushirikiana na Serikali ya Rais Samia ili kuleta mabadiliko ya kudumu katika
kupambana na ukatili, huku wakiwa na lengo la kuhakikisha kuwa jamii inaishi
katika mazingira yenye amani, usawa, na haki.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Nasimama na Mama Popote Nilipo Kanda ya Serengeti, Osca Kaijage,akizungumza na viongozi wa taasisi ya Nasimama na mama mkoa wa Shinyanga.Uongozi
wa Taasisi ya "Nasimama na Mama Popote Nilipo" Mkoa wa Shinyanga
pamoja na viongozi wakanda katika picha ya pamoja baada ya kikao.
Uongozi
wa Taasisi ya "Nasimama na Mama Popote Nilipo" Mkoa wa Shinyanga
pamoja na viongozi wakanda katika picha ya pamoja baada ya kikao.
Uongozi
wa Taasisi ya "Nasimama na Mama Popote Nilipo" Mkoa wa Shinyanga
pamoja na viongozi wakanda katika picha ya pamoja baada ya kikao.
Katibu wa Taasisi ya Nasimama na mama Kanda ya Serengeti, Bw. Renatus Nzemo, akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Nasimama na mama mkoa wa Shinyanga.
Katibu wa Taasisi ya Nasimama na mama Kanda ya Serengeti, Bw. Renatus Nzemo, akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Nasimama na mama mkoa wa Shinyanga.

0 Comments