

Mwenyekiti wa chama cha ACT -Wazalendo Taifa,na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Othman Masoud Othman, amekutana na kufanya mazungumzo na Wadau mbali mbali wa Siasa,kwaajili ya Kujadili Mustakbali wa Demokrasia Nchini.
Kikao hicho kimewajumuisha Wajumbe na Viongozi Wawakilishi wa Vyama Kumi na Saba (17) vya Siasa Nchini, kimefanyika Mei 25,2025 katika Ukumbi wa Hoteli ya Mlashi,ulioko katika Mtaa wa Salunda, Kata ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu.
Mhe.Othman amesema kuwa katika Vita ya Kisiasa na Mapambano ya Kupigania Haki na Demokrasia, suala la umoja, mshikamano na mashirikiano, ni jambo la lazima.
Aidha,kikao hicho kimejumuisha Viongozi, Wajumbe, na Wanachama kutoka Kata zote za Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ndugu Ado Shaibu.
Kikao hicho kimefanyika ukiwa ni muendelezo wa Ziara Maalum inayo fanywa na Mwenyekiti wa chama cha ACT -Wazalendo Taifa,Mhe.Othman Masoud Othman,inayo lenga kuimarisha Harakati za Chama, zilizopewa Jina la 'Operesheni Linda Demokrasia'.
TAZAMA PICHA ZOTE MWENYEKITI ACT-WAZALENDO AKIWA NA VIONGOZI WA VYAMA 17 VYA SIASA SIMIYU.
















0 Comments