6/recent/ticker-posts

ZIC KAHAMA YANOGESHA TABASAMU KWA WATOTO YATIMA KITUO CHA KULELEA WATOTO ZAQAHANA

 

Meneja wa ZIC Kanda ya Magharibi Adam Shomary akizungumza baada ya kutoa msaada katika kituo cha kulelea watoto cha ZAQAHANA kilichopo kata ya Kagongwa Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga

 


Baadhi ya vitu vilivyotolewa na Taasisi ya ZIC kwa Kituo cha Kulelea watoto wanaoishi mazingira magumu cha ZAQAHANA kilichopo manispaa ya kahama mkoani Shinyanga kata ya Kagongwa

Na Samuel Samsoni - Kahama

Taasisi ya Zanzibar Insurance Corporation inayotoa huduma za bima katika Manispaa ya Kahama imeendelea kushirikiana na taasisi na wadau mbalimbali katika kuchangia maendeleo ya jamii kama sehemu ya wajibu wake wa kijamii.

Leo March 13, 2026 taasisi hiyo ilitembelea katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha ZAQAHANA kilichopo kata ya Kagongwa Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga na kutoa msaada wa chakula na vinywaji kama jitihada za kumuunga mkono mmiliki wa kituo hicho na kutambua kazi kubwa anayoifanya ya kuwahudumia watoto wanaoishi katika kituo hicho.

Akizungumza wakati wa utoaji wa msaada huo, meneja wa taasisi hiyo Kanda ya Magharibi Adam Shomary alisema hatua hiyo imetokana na uhitaji mkubwa wa watoto wanaoishi katika kituo hicho baada ya miaka kadhaa nyuma kufuturia, mwaka huu taasisi imeona ipo haja ya kutembelea watoto wanaoishi katika maingira hayo kwa ajili ya kuwapa faraja

“Leo tumeona ni muhimu kutoa msaada maalum katika kituo hiki kwa sababu tulibaini kuwa hapa kuna mahitaji makubwa zaidi, ndiyo maana tumeamua kufika na kuchangia kwa kadri tulivyoweza,” alisema Shomary

Shomary aliongeza kuwa, mwaka huu taasisi hiyo imeelekeza zaidi nguvu zake katika kusaidia watoto yatima baada ya kuguswa na changamoto wanazokutana nazo katika maisha ya kila siku, na kutathmini mahitaji yaliyopo, waliona umuhimu wa kusaidia zaidi idara zinazoshughulika na malezi ya watoto hao ili kuwapa faraja na kuwasaidia kufikia ndoto zao.

Shomary alisema lengo la msaada huo ni kuwajengea matumaini watoto na vijana wanaoishi katika mazingira magumu, hususan wale wasiokuwa na wazazi. Alisisitiza kuwa jamii inapaswa kuwaunga mkono watoto hao ili wajue kuwa bado kuna watu wanaowajali na kuwathamini.

Kwa upande wake, Mfanyakazi katika taasisi hiyo Ziad Haj alieleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za taasisi hiyo kuhakikisha jamii inanufaika na uwepo wake.

“Hii ni sehemu ya wajibu wetu wa kurudisha huduma kwa jamii na kuhakikisha watoto hawa wanapata matumaini ya maisha bora zaidi,” alisisitiza Haj .

Haj ameongeza kuwa jambo hili linaongeza chachu na hamasa kwao kuona kwamba jamii inaweza ikanufaika kutokana na kile wanachokifanya bila kuzingatia ni wateja wao au la!

“Swala zima la kutoa huduma hapa ni kutimiza moja ya majukumu yetu kama taasisi ya kushirikiana na jamii katika shughuli mbalimbali za kijamii na jambo hili linatupa hamasa ya kuona matunda ya kile tunachokifanya kwa jamii.” Alisema Haj.


Mfanyakazi wa taasisi ZIC tawi la Kahama Ziad Haj akizungumza baada ya kutoa msaada katika kituo cha kulelea watoto cha ZAQAHANA kilichopo kata ya Kagongwa Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga

Mlezi wa kituo Madam Zakia Mwambiko alisema kituo hicho kinahudumia watoto sitini na wane (64) waliotoka katika mazingira magumu, wakiwemo waliopoteza wazazi au waliotelekezwa na kuwa watoto hao wanahitaji malezi, elimu pamoja na huduma za afya ili waweze kukua katika mazingira salama.

Alisema kituo hicho kimekuwa kikikabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za chakula, malazi na matibabu, hivyo msaada kutoka kwa wadau mbalimbali umekuwa ukisaidia kupunguza changamoto hizo.

“Tunawashukuru sana wadau wanaoendelea kutusaidia kwa hali na mali, kwa sababu watoto hawa wanahitaji upendo na msaada wa jamii,” alisema Madam Zakia.

Alisema kuwa licha ya changamoto zilizopo, kituo hicho kinaendelea kuhakikisha watoto wote wanafikia umri wa kwenda shule wanapata elimu. Alisema elimu ni silaha muhimu itakayowasaidia watoto hao kujitegemea na kuwa sehemu yenye mchango chanya katika jamii.

“Watoto wote wenye umri wa kwenda shule nimewapeleka shuleni, kwahiyo hapa wapo watoto wa chekechea mpaka Sekondari” Amesema Mwambiko

Alitoa wito kwa wadau, taasisi na watu binafsi kuendelea kushirikiana na kituo hicho ili kuboresha maisha ya watoto hao kupitia ujenzi unaoendelea wa nyumba yakuishi watoto hao ambao uko hatua ya lenta na ukihitaji nguvu zaidi kutoka kwa wadau mbali mbali wa maendeleo.
Madam Zakia Mwambiko Mmiliki wa kituo cha kulelea watoto wanaoishi mazingira magumu cha ZAQAHANA kilichopo kata ya Kagongwa Manispaa ya kahama mkoani Shinyanga akizungumza baada ya kupokea misaada hiyo


Awali akizungumza Sheikh Nasor kutoka Msikiti wa Ibadh uliopo Kahama Manispaa alisema jambo hili ni jambo kubwa sana katika ibada na kwamba yule anayekataa dini ni yule anayemfukuza yatima na hahamasishi kuwalisha masikini.

"Kusali na kuinuka siyo dini peke yake, dini ina mfumo wake kama mwenyezi Mungu Allah Subhanahu wa Ta’ala anavyoelekeza, hivyo jambo hili ni zuri sana na tunamuomba mwenyei Mungu alikuze katika staili ambayo anaijua yeye tu” Alisema Sheikh Nasor

Alisisitiza kuwa kusaidia watoto yatima ni ibada kubwa inayosisitizwa katika mafundisho ya dini ya Kiislamu. Akiongeza kuwa wanaendelea kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema ya kuwasaidia wengine na kumuomba awabariki, awape nguvu ya kuendelea kufanya mema, awaponye wagonjwa na kuwarehemu waliotangulia mbele ya haki.
  • Sheikh Nasoro kutoka Msikiti wa Ibadh uliopo Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga akizungumza pamoja na kufanya dua wakati wa utoai wa msaada huo
Muonekano wa jengo linalojengwa kama kituo cha kulelea watoto hao kata ya kagongwa Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga

Baadhi ya watoto wanaoishi katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha ZAQAHANA kilichopo kata ya Kagongwa Manispaa ya kahama Mkoani Shinyanga

Baadhi ya watoto wanaoishi katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha ZAQAHANA kilichopo kata ya Kagongwa Manispaa ya kahama Mkoani Shinyanga







Baadhi ya watoto wanaoishi katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha ZAQAHANA kilichopo kata ya Kagongwa Manispaa ya kahama Mkoani Shinyanga















Post a Comment

0 Comments