Mhita ametoa wito huo wakati akizindua rasmi kimkoa awamu ya pili ya usajili wa Bima ya Afya kwa Wote, zoezi ambalo limefanyika leo tarehe 22 Oktoba, 2026, kwenye Uwanja wa Zimamoto, Manispaa ya Shinyanga, katika hafla iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya afya wakiwemo wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Shinyanga, Wakurugenzi wa Halmashauri na wananchi.
| Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita |
Mkuu huyo wa mkoa amebainisha kuwa, katika kuhakikisha watanzania wote wanapata huduma bora za afya na kwa gharama nafuu, Serikali ya awamu ya Sita inaoyoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imefanya mapinduzi makubwa katika Sekta ya afya, ambapo imeanza kwa kuboresha miundombinu ya Sekta hiyo kwa kujenga zahanati, vituo vya afya na Hospitali za wilaya, mikoa na za rufaa.
Pia, imenunua vifaa tiba vya kisasa pamoja na kuajiri kwa wingi wataalam wa afya wakiwemo madaktari bingwa na wabobevu pamoja na kuwaendeleza kiujuzi wale waliokuwa kwenye vituo vya kazi.
Mhita amewasisitiza wananchi wote kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kujisajili kwenye bima ya afya kwa wote, ili wanapate huduma za afya bila kikwazo na kwa gharama nafuu ya Shilingi laki moja na Elfu Hamsini kwa mwaka, kwa watu Sita kwenye familia inayojumuisha mwanachama mchangiaji, mweza wake na watoto wanne.
Mhita ameahidi kusimamia utekelezaji wa zoezi hilo ili likamilike kama ilivyokusudiwa na Serikali, ambapo ametumia nafasi hiyo kuwaagiza wakuu wa wilaya kushirikiana na wakurugenzi wa halmashauri kuratibu kwa karibu shughuli zote za usajili.
Aidha, amewataka watumishi wote wanaohusika zoezi hilo kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na weledi na kwamba, watoa huduma za afya wahakikishe wananchi waliojiunga na bima ya afya kwa wote wanapata huduma kwa wakati, bila usumbufu na kwa kiwango kinachostahili.
Mkuu huyo wa mkoa wa Shinyanga, pia amewataka wakurugenzi wa Halmashauri kushirikiana na watendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na wadau wengine ikiwemo vyombo vya habari, kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi, ili waelewe umuhimu wa bima hiyo na kujisajili.
Mhita pia amewaomba viongozi wa dini, viongozi wa kimila, wafanyabiashara na viongozi wa makundi mbalimbali ya kijamii kutumia mikusanyiko yao kuhamasisha wananchi kujiunga na mpango huo.
Kwa upande wake, Afisa Mipango Mkuu wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Kanda ya Magharibi, Ahimidiwe Asseri, amesema mamlaka hiyo italinda maslahi ya wanachama kwa kuhakikisha wanapata huduma kulingana na vifurushi walivyochagua.
| Afisa Mipango Mkuu wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Kanda ya Magharibi, Ahimidiwe Asseri |
Bw. Asseri amewataka wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka hiyo wanapokumbana na changamoto au mapungufu katika utoaji wa huduma.
| Meneja wa NHIF Mkowa wa Shinyanga Franklin Chekani |
| Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Anord Makombe akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM mkoa Mabala Mlolwa |
| Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akiwasalimia wananchi na kumkaribisha Mgeni rasmi kwa ajili ya kuzungumza |
| Watatu katikati ni wakuu wa Wilaya za mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye uzinduzi |
| Mwenye Koti katikati ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt. Luzila John |
| Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Pili Mnyami |
| Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Honoratha Rutatinisibwa |
0 Comments