6/recent/ticker-posts

ASILIMIA 75% YA MAFANIKIO YA WANAUME YANA NGUVU YA MWANAMKE.

Saimon Laizer Makamu Askofu kanisa la IEAGT Tanzania Kutoka mkoani Arusha akifungua kongamano la kitaifa la wanawake  wakanisa la IEAGT.

Na.Amo Blog Shinyanga.

Jamii imetakiwa kuondokana na mitazamo hasi ya kuwatambua wanawake kama viumbe dhaifu badala yake watambue na kuthamini mchango wawanawake katika kuchochea maendeleo ya familia ,jamii na Taifa kwa ujumla.

Makumu Askofu wa Kanisa la IEAGT Tanzania Askofu  ,Saimon Laizer ameyasema hayo leo septemba 12,2023 wakati akifungua kongamano la Kitaifa la wanawake wa Kanisa la IEAGT litakalofanyika kwa siku 5 kwa ajili kuelimisha wanawake kuhusu malezi na makuzi,uchumi na ushiriki kwa ajili ya huduma za kanisa.

Askofu Laizer anasema,uwepo  wa Mitazamo,mila na desturi zilizopitwa na wakati  zimewafanya baadhi ya wanawake kuoneka kuwa ni watu wa chini na wasioweza jambo lolote katika jamii.

Askofu Laizera mesema kuwa Dunia katika karne ya 21 isiendele kuwa chukualia wanawake kuwa ni watu wa chini na hawezi kufanya jambo lolote juu ya maendeleo badala yake watambue na kuthamini mchango walio nao katika kuchochea maendekei ya familia, jamii kanisa na Taifa kwa ujumla.

"Tumeendelea kuwaweka chini wanawake ila maendeleo  mengi ya kaninsa na familia wao wanamchango mkubwa zaidi kwa jitihada zao,Ukweli ni kuwa asilimia  75% ya mafanikio ya wanaume yana nguvu ya wanawake na ukitaka kuona umuhimu wao akisafiri uwa nyumba inakuwa haieleweki na wanaume kuona kuna kupwaya juu ya nafasi yake"amesema Laizer

Pia Askofu Laizer amewasii  wanawake wakabisa hilo kuwajibika kiimani katika kutetea familia,kanisa na Taifa kwa kuomba na kusali wakiziombea familia zao ,kanisa na Taifa la Tanzania.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wanawake Taifa ,Suzana Mabushi amewataka Wanawake wakanisa hilo kujiepusha na tabia zisizo faa ikiwemo kujikatia tamaa na kuwanenea mabaya watoto wao " amesema Suzan Mabushi .
Saimon Laizer Makamu Askofu kanisa la IEAGT Tanzania Kutoka mkoani Arusha akifungua kongamano la kitaifa la wanawake  wakanisa la IEAGT.
Askofu wa kanisa la IEAGT Tanzania Askofu David Mabushi akizungumza wakati wakufungua kongamano la kitaifa la wanawake  wakanisa la IEAGT.


Post a Comment

0 Comments