6/recent/ticker-posts

KAMPENI YA TUWAJIBIKE YAFANA SHINYANGA, DC SAMIZI APONGEZA AONGOZI WA TRA KWA KUFANYA MATEMBEZI YA KUHAMASISHA WAFANYABIASHARA KUTOA RISITI HALALI ZA MAUZO YA BIDHAA KWA WATEJA

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi ambaye alikuwa Mgeni Rasmi kwenye kampeni ya Tuwajibike akibandika kaulimbiu ya kampeni kwenye duka la mmoja wa wafanyabiashara mjini Shinyanga.

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

 

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA)Mkoa wa Shinyanga wamehitimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kuendeleza Kampeni ya Uwajibikaji ya kutoa na kudai Risiti halali kwa Wafanyabiashara na Wananchi, ili Serikali ipate mapato sahihi, fedha ambazo zitatumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.TRA wamehitimisha wiki hiyo ya huduma leo Oktoba 6, 2023,ambayo ilianza Oktoba 3, kwa kufanya matembezi ya kutembelea baadhi ya Wafanyabiashara kwenye maduka yao na kuwapatia elimu ya kutoa Risiti halali kwa wateja, pamoja na kuzungumza na Wananchi juu ya umuhimu kudai Risiti halali za manunuzi ya bidhaa zao.Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi ambaye alikuwa Mgeni Rasmi kwenye matembezi hayo, amewasihi Wafanyabiashara kuendelea kulipa kodi za Serikali kwa hiari na kutoa Risiti halali za mauzo ya bidhaa zao kwa wateja, pamoja na wananchi kudai Risiti halali, hali ambayo Serikali itapata mapato halisi.

Amesema nchi yoyote ambayo imepiga hatua kimaendeleo wananchi wake ni walipaji wa kodi wazuri, na kuwasihi Wafanyabiashara wasikwepe kulipa mapato ya Serikali, bali walipe kwa hiari yao kwa maendeleo ya Taifa pamoja na kutoa Risiti halali za mauzo ya bidhaa zao kwa wateja na siyo kuiibia Serikali.

 “Ulipaji kodi ndiyo msingi wa maendeleo ya Taifa letu, fedha ambazo zimekuwa zikipatikana ndizo hizi ambazo hutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo na miradi ya kimkakati,”amesema Samizi.

Aidha, amewataka pia wananchi kukataa tabia ya baadhi ya Wafanyabiashara kuwapatia Risiti za kusindikiza mzigo, ambazo hazina uhalisia wa kiwango halisi cha fedha ambazo wamenunua bidhaa zao na kuiibia mapato Serikali.

 Naye Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga Faustine Mdessa, amesema wiki hiyo ya mlipa kodi wameitumia vizuri kutoa elimu kwa Wafanyabiashara na kutengeneza mahusiano mazuri, na kuwasihi juu ya ulipaji kodi kwa hiari na utoaji Risiti halali kwa wateja, fedha ambazo huwarudia kupitia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

 “Faida ya utoaji na kudai Risiti halali ni kuisaidia Serikali kupata mapato sahihi,”amesema Mdesa.

Nao baadhi ya Wafanyabiashara mkoani Shinyanga akiwamo Warda Omary, wamesema wanafahamu faida za ulipaji kodi na wameona maendeleo makubwa ambayo yamekuwa yakifanywa na Rais Samia, na kutoa wito kwa Wafanyabiashara ambao 









Post a Comment

0 Comments