6/recent/ticker-posts

RC MNDEME AWAELEZA WATENDAJI WAKATA NA VIJIJI UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO, WATENDAJI WAMPONGEZA KWA KUWAPA MBINU ZA KUPAMBANA NA VITENDO VYA UKATILI



Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme akiwa katika  kikao kazi na Maafisa Tarafa, watendaji kata, mitaa na vijiji

Na Amo Blog Shinyanga

MKUU wa mkoa wa shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme amefanya kikao kazi na Maafisa Tarafa, watendaji kata, mitaa na vijiji kwa lengo la kuwakumbusha majukumu yao ya kazi ikiwemo kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, utatuzi wa kero za wananchi, kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato, kueleza umma juu ya fedha wanazopokea kutoka serikali kuu, utunzaji wa mazingira na kupambana dhidi ya ukatili wa kijinsia katika maeneo yao.

Mhe. Mndeme ameyasema hayo leo tarehe 10 Oktoba, 2023 wakati alipokutana na wataalam hao katika ukumbi wa mikutano uliopo shule ya savannah plains huku akiwasisitiza kwenda kuzingatia maadili na nidhamu huku akikemea tabia ya kuchati na simu wanapokuwa wakiwahudumia wananchi huku akisisitiza kuwa kipaumbele cha serikali ni utoaji wa huduma bora kwa wananchi wenyewe na ndiyo maelekezo ya Mhe. Rais.

"Nendeni mkasimamie utekelezaji wa miradi ya maendeleo, mkatoe elimu juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira, tatueni kero za wananchi, toeni taarifa za mapokezi ya fedha za serikali pia mkaongeze bidii katika kukusanya wamapato ya serikali katika maeneo yenu," alisema Mhe. Mndeme.

Katika hatua nyingine Mhe. Mndeme amewaeleza wataalam hao kuwa serikali ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeleta zaidi ya Trilioni moja fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali huku akiwataka kwenda kuzisimamia ili zililete matokeo chanya kwa wananchi katika maeneo yao

Aidha amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote za mkoa huu kuhakikisha wanalipa stahiki za watumishi wao, kuandaa mafunzo ya watumishi, kutatua kero za wananchi na watumishi katika halmashauri zao ili wamsaidie Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ndiyo maelekezo yake huku akiwataka kuchapa kazi kwa bidiii zaidi

 Kwa upande wao wakurugenzi wa halmashauri hizi za mkoa wa shinyanga wamekiri kupokea maelekezo ya Mhe. Mndeme na kumuahidi kuwa wanakwenda kuyatekeleza maelekezo yote ikiwemo utatuzi wa migogoro na kulipa stahiki za watumishi wao.



Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Profesa Siza Tumbo  akizungumza katika kikao kazi


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza katika kikao kazi.


Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwl.Kagunze  akizungumza katika kikao kazi.

Maafisa Tarafa, watendaji kata, mitaa na vijiji wakiwa kwenye kikao kazi.

Maafisa Tarafa, watendaji kata, mitaa na vijiji wakiwa kwenye kikao kazi.


Maafisa Tarafa, watendaji kata, mitaa na vijiji wakiwa kwenye kikao kazi.
Maafisa Tarafa, watendaji kata, mitaa na vijiji wakichangia mawazo yao kwenye kikao kazi.

Post a Comment

0 Comments