6/recent/ticker-posts

WAFANYAKAZI WA NSSF SHINYANGA WAJUMUIKA NA WANACHAMA KATIKA UFUNGUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA 2023

Meneja wa NSSF Mkoa wa Shinyanga Amina Mdabi akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya huduma kwa wateja mkoani Shinyanga.

Na.Amo Blog Shinyanga

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi amefungua rasmi Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kukata na kula keki na wanachama  na wafanyakazi wa NSSF Mkoa wa Shinyaga.

Akizungumza mapema hii leo Jumatatu Oktoba 2,2023 wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, Meneja wa NSSF mkoa wa Shinyanga Amina Mdabi amesema kuwa wiki ya huduma kwa wateja ilianzishwa rasmi kimataifa mwaka 1984 kwa lengo la kutambua umuhimu wa huduma bora kwa wateja na juhudi za wafanyakazi wanao toa huduma bora kwa wateja.

“Wiki ya Huduma kwa Wateja hufanyika kila mwaka kimataifa kuanzia  Oktoba 2.NSSF mkoa WaShinyanga tunaitumia wiki hii kutafakari juu ya huduma tunazotoa, kusikiliza wateja na wadau mbalimbali,Kauli mbiu ya Wiki ya Huduma kwa wateja mwakahuu ni ‘’Ushirikiano kwa huduma bora”,amesema Mdabi.

Mdabi amemshukuru Rais wajamhuri wa muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye ni mtoa huduma namba moja kwa juhudi kubwa anazo fanya na anazo endelea kuzifanya katika kuhakikisha anaboresha huduma kwa jamii huku akiwaomba wanachama wa NSSF na waTanzania kuunga mkono jitihada hizo zinazo fanya na Dkt.Samia.

Aidha Mdabi amewashukuru wanachama Wamfuko wa NSSF mkoa wa Shinyanga kwa kuendelea kuwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kuwaomba wajasiriamali kujiunga na NSSF Ili waweze kujiwekea Mafao kidogokidogo yatakayo wasaidia uzeeni.

Pia tuna mshukuru Mkurugenzi mkuu na bodi ya wadhamini kwa namna ambavyo wameweza kuboresha utendaji kazi kwa kutumia Teknoloji hali ambayo kwa sasa imeasaidia kuhudumia wateja kwa ufanisi.

 Kwa upande wao baadhi ya wanufaika wa  Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)mkoa wa Shinyanga akiwemo Dorica Bushu na John Ndama wamesema wataendelea kuwa mabalozi wakutoa elimu kwa watu wengine ambao bado awajajiunga na mfuko huo  wakiwemo wajasiriamali na wananchi ili waweze kujiwekea fedha kidogokidogo kwa ajili ya maisha yao ya baadae.

Meneja wa NSSF Mkoa wa Shinyanga Amina Mdabi akikata keki wakati wa ufunguzi wa wiki ya huduma kwa wateja NSSF Shinyanga.











Mnufaika wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dorica Bushu akizungumza wakati wa zoezi hilo la ufunguzi.


Meneja wa NSSF Mkoa wa Shinyanga Amina Mdabi (kulia) akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wanufaika wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa ufunguzi wa wiki ya huduma kwa wateja mkoani Shinyanga.









Post a Comment

0 Comments