6/recent/ticker-posts

UONGOZI CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOCU SHINYANGA ,CHANZO CHA WANAFUNZI KUFANYA VIZURI KITAALUMA NA KIMICHEZO

Washindi katika mchezo wa fainali Diproma ya kwanza wakionyesha furaha yao baada ya kuchukua zawadi ya Ng'ombe mnyama katika fainali hiyo wakiifunga timu ya Diproma mwaka wapili.

Na Amo Blog Shinyanga.

Uongozi wa serikali ya wanafunzi MoCUSO  Katika chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Tawi la Kizumbi mkoani Shinyanga umetoa pongezi kwa uongozi wa chuo hicho kwa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia pamoja na kutoa fursa ya wanachuo kuonyesha vipaji vyao .

Hayo yameelezwa na baadhi ya wanafunzi wachuo Kikuu cha Ushirika Moshi Tawi la Kizumbi mkoani Shinyanga akiwemo makamu wa Rais wa Chuo hicho Benson Mhanga wakati wa mchezo wafainali ulio chezwa katika uwanja wa chuo hicho Januari 9 ,2024 ukiikutanisha Timu ya Diproma mwaka wa kwanza na Timu ya  Diproma Mwaka wapili kozi ya Uhasibu na Utawala.

Aidha Bw. Benson Mhanga makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi MoCUSO amesema kuwa uwepo wa uongozi bora wawa kufunzi katika chuo hicho imesaidia kuinua kiwango cha Taaluma kwa wanafunzi pamoja na kuinua vipaji wa wanamichezo katika chuo hicho maana wanafunzi wamekuwa na utamaduni wa kupewa mda wakufanya michezo baada ya masomo ya darasani.

‘Tunawashukuru sana wakufunzi wetu kwa kutupa mda wa kuonyesha vipaji vyetu baada ya mda wa darasani , na kama unavyoona wanafunzi wamepata nafasi ya kuburudika lakini pia kubadilishana mawazo’ alisema Benson.


Wachezaji Diproma ya kwanza wakijiandaa na mchezo.

Wachezaji Diproma ya pili wakijiandaa na mchezo.

Mashabiki wakifurahia burudani.
Mashabiki wakifurahia burudani.
Mashabiki wakifurahia burudani.







































Post a Comment

0 Comments