6/recent/ticker-posts

MENEJA WA KACU KAHAMA NA VIONGOZI 8 WA AMCOS WABURUZWA MAHAKAMANI NA TAKUKURU SHINYANGA KWA TUHUMA ZA WIZI WA FEDHA ZAWAKULIMA


Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga Donasy Kessy akitoa taarifa kwa waandishi wa habari


Na mwandishi wetu.


Viongozi nane (8) wa Chama kikuu Cha ushirika Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga (KACU) na wengine kutoka Chama Cha msingi Kangeme wamefikishwa mahakamani na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga kwa vitendo vya rushwa na kuhamisha fedha.


Hayo ameyasema leo jumatano 31,2024 mkuu wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga Donasy Kessy alipokuwa akitoa taarifa kwenye vyombo vya habari katika kipindi cha Miezi mitatu kuanzia April hadi Juni mwaka 2024, ambapo amesema viongozi hao wamefikishwa mahakamani ili kujibu mashtaka yao.


Kessy amesema kesi nne zinaendelea kusikilizwa na kesi moja ya Jamhuri iliyokuwa Inamhusu Meneja Mkuu wa KACU Abdul Ally wengine Juma Simon na Emannuel Shoboga wote watumishi wa KACU waliamriwa kulipa faini ya shilingi Milioni tatu na kifungo cha nje miezi sita.


Kessy amesema kesi iliyokuwa ikisimamiwa na Jamhuri ilishinda na watuhumiwa wameamriwa kulipa shilingi Milioni 24 walizozipata kwa njia ya rushwa na tayari shilingi Milioni 12 zimerejeshwa.


Kessy amesema walichobaini viongozi hao walitoa fedha kwenye akaunti za chama nakuzigawana kupitia akaunti zao binafsi ,kughushi delivery note,invoice na kufanyika kwa malipo yasiyo halali kwa madai ya kulipa wafanyabiashara walioleta pembejeo kwenye Amco's.


"Tuhuma zingine walizokutwa nazo viongozi ni kukopa fedha benki kupitia Amco"s na kuzitumia kwa matumizi yao binafsi na mkopo kulipwa hali iliyopelekea chama kushindwa kuwalipa wakulima fedha za mauzo ya Mazao" amesema Kessy.


Aidha Kessy amesema baada ya kufanya ufuatiliaji na malalamiko ya madeni ilibaini vyama vya msingi 13 vina madeni yaliyosababishwa na kughushi delivery notes,invoice na kufanyika kwa malipo yasiyo halali kwa wafanyabiashara walioleta pembejeo kwenye (Amco's).


"Takukuru inaendelea kufanyia kazi malalamiko ya wanachama katika vyama vingine kumi na moja la vyama vya Msingi na kuhakikisha hatua stahiki za kisheria zinachukuliwa kwa viongozi wote waliojihusisha na vitendo vya rushwa"alisema Kessy.


"Na hii itakuwa fundisho kwa vionhozi wa AMCOS na vyama vikuu vya ushirika vingine waache kufuja mali na fedha za vyama, serikali kupitia Takukuru itahskikisha wote wanaofilisi mali na fedha za wakulima wanashughulikiwa kwa mujibu wa sheria"ameongeza.


Pia Takukuru imefuatilia miradi ya maendeleo miwili ya sekta ya elimu na kilimo inayotekelezwa katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Kishapu yenye thamani ya Shilingi Bilioni 11,308, 291,500.


Takukuru imeendelea kuxiba misnya ya rushwa kwenye mfumo wa uwasilishaji wa kodi za zuio katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mfumo wa utoaji wa ardhi na mfumo wa uendeshaji wa jumuiya ya watumiaji maji CBWSO za hslmashauri ya Kishapu .


Aidha dawati la uchunguzi, limepokea malalamiko 46 kati ya hayo, malalamiko yaliyohusu rushwa yalikuwa 28 na uchunguzi wake unaendelea malalamiko yasiyohusu rushwa 18 na kesi zinazoendelea mahakamani ni 17, kesi mpya tisa na kati ya hizo jamhuri ilipata ushindi wa kesi 1 na kesi iliyoshinda ni kesi moja.


Post a Comment

0 Comments