6/recent/ticker-posts

MHE.KATAMBI APELEKA FURAHA KWA TIMU YA UPONGOJI STAR ,MAARUFU KAMA WARABU WA YEMENI MASEKELO SHINYANGA ,UONGOZI WA TIMU WAMPA WAMPA BIG UP KATAMBI

Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mhe.Patrobas Katambi amekabidhi zawadi ya jezi ,mpira na zawadi mbalimbali kwa timu ya Upongoji Star maarufu kama warabu wayemeni ikiwa nisehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama chamapinduzi kwa kuimarisha maendeleo katika sekta ya michezo jimboni humo.

Mhe.Katambi ambaye ni mbunge wajimbo la Shinyanga amekabidhi zawadi hizo Augost 12 ,2024 kwa timu hiyo ikiwani sehemu ya kutimiza ahadi yake aliyo ahidi wakati waziara ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Benard Werema. 

Aidha Mhe.Katambi ameogeza kuwa ameamua kukabidhi zawadi hizo ikiwani sehemu ya kuunga mkono jitihada zatimu hiyo yenye hamasa ndani ya Manispaa ya Shinyanga na kuendeleza soka la vijana wajimbo la Shinyanga na mkoa kwa ujumla.

Kwa upande wake Katibu Msaidizi wa Timu hiyo Halima Kambi akizungumza kwaniaba ya viongozi na wanachama wa timu hiyo amempongeza Mhe.Katambi kwa kuwapa msaada huo ambao utasaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa vifaa vya michezo katika timu yao huku wakiahidi kuendelea kuunga mkono juhudi zinazo fanywa na viongozi wa Serikaki ya awamu ya sita katika kuchochea maendeleo nakuahidi kuendelea kufanya vizuri katika sekta ya michezo kwa kuwa tayari changamoto iliyo kuwa ikiwakabili vijana hao tayari imetatuliwa na mbunge wa jimbo hilo.

Post a Comment

0 Comments