6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI KATAMBI ASHIRIKI MAPOKEZI YA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MANISPAA YA SHINYANGA ,ATOA MAAGIZO MIRADI 13 ILIYO KATALIWA NA MWENGE NCHINI

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Paschal Katambi, ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini akizungumza katika hafla ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa shule ya msingi Ibadakuli leo Jumapili Agosti 11,2024.

Na Mapuli Kitina

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Paschal Katambi, amesema kuwa Mwenge wa Uhuru umekimbia katika mikoa zaidi ya 22 na kukagua miradi 1,074 yenye thamani ya shilingi trilioni 10.7.

Katika miradi hiyo, miradi 13 yenye thamani ya shilingi bilioni 7.6 imekutwa na dosari mbalimbali na kwamba Mwenge wa Uhuru umepita kwenye Halmashauri 131 na bado unatarajiwa kufika katika Halmashauri 64 kati ya 195 zilizopangwa.

Mhe. Katambi amesema kuwa miradi iliyo na dosari tayari imechukuliwa hatua stahiki na mamlaka husika zimepewa maagizo ya kuirekebisha mara moja.

Miongoni mwa miradi iliyokutwa na dosari ni mradi wa maji katika Manispaa ya Morogoro, pamoja na miradi mingine iliyopo mikoa ya Njombe, Dodoma, Singida, Mara, na Itilima mkoani Simiyu.

Mhe. Katambi ameongeza kuwa serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria na kiutawala dhidi ya watumishi wa umma watakaobainika kuhusika na kasoro hizo.

"Hatutasita kuchukua hatua kali za kisheria na kiutawala pale ambapo mradi utapata dosari na watumishi wa umma wamehusika," amesema Mhe. Katambi,

Amesisitiza kuwa fedha zilizotolewa na serikali zinapaswa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi bila kuleta hasara yoyote.

Mwenge wa Uhuru unaendelea na kazi zake katika mikoa na Halmashauri zilizobaki, ukilenga kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa inakaguliwa na kuhakikisha inatoa huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Paschal Katambi, ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini akizungumza katika hafla ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa shule ya msingi Ibadakuli leo Jumapili Agosti 11,2024.

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Paschal Katambi, ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini akizungumza katika hafla ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa shule ya msingi Ibadakuli leo Jumapili Agosti 11,2024.

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Paschal Katambi, ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini akizungumza katika hafla ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa shule ya msingi Ibadakuli leo Jumapili Agosti 11,2024.

TAZAMA HAPA CHINI PICHA ZA LEO KWENYE MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU MANISPAA YA SHINYANGA

Post a Comment

0 Comments