6/recent/ticker-posts

UWT MASEKELO WAPONGEZA USHIRIKI WA WANAWAKE UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA, WAIPONGEZA CCM KUMPA SAMIA MITANO TENA

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Tawi la Masekelo, Kata ya Masekelo, Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Amina Francis Mwandu akiteta jambo na Katibu wa UWT Tawi la Masekelo bi. Pendo Zabron (kushoto)

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Tawi la Masekelo, Kata ya Masekelo, Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Amina Francis Mwandu akizungumza kwenye mkutano wa UWT tawi la Masekelo

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Tawi la Masekelo, Kata ya Masekelo, Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Amina Francis Mwandu, amewapongeza wanawake wa Masekelo kwa kushiriki kwa nguvu zote katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika tarehe 27 Novemba, 2024, huku akiwaomba kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, 2025.

Pongezio hizi amezitoa leo, Jumatano, Januari 22, 2025, wakati wa mkutano wa kuwashukuru wanawake wa tawi hilo kwa ushiriki wao mzuri katika uchaguzi wa serikali za mitaa. 

Mkutano huo pia ulilenga kufanya tathmini ya shughuli zilizopita na kuelezea mipango mbalimbali wanayoendelea nayo, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wanawake kujisajili kwa mfumo wa kielektroniki ili kuwa wanachama hai wa UWT.

"Kwa niaba ya UWT tawi la Masekelo, tunawashukuru na kuwapongeza sana wanawake kwa ushirikiano mkubwa mliouonesha katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Mlijitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi, mkashiriki kuchagua viongozi wa CCM, na kama matokeo yake yalivyo, CCM ilipata ushindi wa kishindo. Wanawake ni jeshi kubwa, na tunaweza. Mlijitokeza kwa wingi kutokana na kampeni ya hamasa ambayo UWT na chama kwa ujumla ilifanya nyumba kwa nyumba," amesema Bi. Amina.

Aidha, Bi. Amina amewahimiza wanawake kuendelea kujisajili katika mfumo wa kielektroniki ili kuwa wanachama hai wa UWT, na pia kulipia ada za uanachama wa CCM.

"UWT tawi la Masekelo inaendelea kupokea wanachama kila siku. Naomba muendelee kujisajili UWT kwa mfumo wa kielektroniki na kuwa Wana Chama hai wa UWT. Pia, tunawakaribisha wale ambao bado hawajajiunga na CCM kujiunga, na kama una jirani au ndugu ambaye bado hajajiunga, mhamasishe aje tumsajili ili awe na kadi ya CCM",ameongeza Amina.

 Amina Francis Mwandu 

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo wa UWT amekishukuru na kukipongeza Chama Cha Mapinduzi kwa kumchagua Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kugombea Urais wa Tanzania mwaka huu kwa Tiketi ya CCM. 

Bi. Amina ameeleza kuwa Rais Samia ni kiongozi mahiri ambaye ameleta maendeleo makubwa nchini, na kwamba wanawake wa Masekelo wanamuunga mkono kwa dhati.

"Pia, tunawaomba akina mama kuwa mstari wa mbele kufichua vitendo vya ukatili wa kijinsia katika familia na jamii kwa ujumla. Lengo letu ni kuwa na jamii salama, yenye kuheshimu haki za binadamu," amesisitiza.

Kwa upande wake, Katibu wa CCM Tawi la Masekelo, Kata ya Masekelo, Monica Stanley, amewataka wanawake kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu, akihamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi katika uchaguzi huo, pamoja na kuchagua Madiwani, Wabunge, na Rais kutoka CCM.

Naye Katibu wa UWT Kata ya Masekelo, Bi. Mwanahamisi Kazoba, amesisitiza kuwa CCM ina kila cha kujivunia kutokana na maendeleo makubwa yaliyofanywa chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akitolea mfano ujenzi wa zahanati katika kata hiyo, madarasa na kuboresha miundombinu ya barabara.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Tawi la Masekelo, Kata ya Masekelo, Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Amina Francis Mwandu akizungumza kwenye mkutano wa UWT tawi la Masekelo
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Tawi la Masekelo, Kata ya Masekelo, Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Amina Francis Mwandu akizungumza kwenye mkutano wa UWT tawi la Masekelo
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Tawi la Masekelo, Kata ya Masekelo, Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Amina Francis Mwandu akizungumza kwenye mkutano wa UWT tawi la Masekelo
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Tawi la Masekelo, Kata ya Masekelo, Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Amina Francis Mwandu akizungumza kwenye mkutano wa UWT tawi la Masekelo
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Tawi la Masekelo, Kata ya Masekelo, Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Amina Francis Mwandu akizungumza kwenye mkutano wa UWT tawi la Masekelo
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Tawi la Masekelo, Kata ya Masekelo, Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Amina Francis Mwandu akizungumza kwenye mkutano wa UWT tawi la Masekelo. Kushoto ni Katibu wa CCM Tawi la Masekelo, Kata ya Masekelo, Monica Stanley akifuatiwa na Katibu wa UWT Tawi la Masekelo bi. Pendo Zabron
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Tawi la Masekelo, Kata ya Masekelo, Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Amina Francis Mwandu na Katibu wa UWT Tawi la Masekelo bi. Pendo Zabron (kushoto) wakiwa kwenye mkutano
Katibu wa UWT Tawi la Masekelo bi. Pendo Zabron akimkaribisha Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Tawi la Masekelo, Kata ya Masekelo, Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Amina Francis Mwandu kwenye mkutano
Katibu wa CCM Tawi la Masekelo, Kata ya Masekelo, Monica Stanley akuzungumza kwenye mkutano huo
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Masekelo Rehema Kategire akizungumza kwenye mkutano huo
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Masekelo Elizabeth John akizungumza kwenye mkutano huo
Katibu wa UWT Kata ya Masekelo, Bi. Mwanahamisi Kazoba  akizungumza kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Tawi la Masekelo, Kata ya Masekelo, Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Amina Francis Mwandu (katikati aliyevaa miwani na nguo ya kijani) akicheza muziki na wanawake wa Masekelo

Post a Comment

0 Comments