
Mkurugenzi wa Taasisi ya DadaHood Initiative na mtangazaji maarufu kutoka Clouds FM, Mkuwe Issale (MAMYBABY), amekitumia tamasha la The Orange Concert kutoa elimu ya kiuchumi kwa wanawake na wasichana.
Tamasha hilo limefanyika katika ukumbi wa RISTALEMI HOTEL mkoani Tabora, ikiwa na lengo la kuwajengea ujuzi, maarifa, na uzoefu wanawake kutoka kwa watoa mada mbalimbali wa ndani ya mkoa wa Tabora na nje ya mkoa akiwemo muigizaji maarufu Irene Paul.
Akizungumza katika Tamasha hilo, Mkuwe Issale amesisitiza umuhimu wa wanawake kuchangamkia fursa za kiuchumi na kujitahidi kujikwamua kiuchumi ilikuepuka kuwa tegemezi katika familia jamii na Taifa kwa ujumla hali itakayo saidia wanawake wengi mkoani humo kuwa na maisha bora .
Aidha Mkuwe ametumia nafasi hiyo kuwashawishi wanawake kujitokeza kwa wingi katika masuala ya siasa, ili kuwakilisha maslahi ya wanawake katika ngazi za uongozi.
Naye Irene Paul, ambaye ni miongoni mwa waigizaji maarufu katika tasnia ya filamu ya Tanzania, amezungumza na wanawake wa mkoa huo kuhusu umuhimu wa kujitambua, kujimudu kiuchumi, na kujenga uwezo wa kiakili na kuthamini bidhaa wanazo zarisha ili kufikia malengo yao.
"Usawa katika jamii ni muhimu, na wanawake lazima wawe sehemu ya mabadiliko. Ili kufikia mafanikio yoyote, ni lazima tuwe na imani na uwezo wetu wenyewe. Ninyi ni nguvu kubwa," alisema Irene Paul, akionyesha kujitolea kwake kuunga mkono maendeleo ya wanawake.
Semina hiyo imevutia wanawake wengi kutoka kila pembe ya Tabora, huku wakiwa na shauku ya kujifunza zaidi kuhusu njia bora za kuboresha maisha yao na familia zao. Irene pia alisisitiza umuhimu wa elimu ya kifedha, kujengeana mrejesho mzuri, na kujiamini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Bandora Mirambo, ametumia nafasi hiyo kukemea vikali tabia ya mfumo dume unaowaathiri wanawake na watoto wa kike katika jamii kwa kulaani tabia ya baadhi ya wanaume wano wakataza wake zao na watoto wa kike kushiriki katika biashara na shughuli za kiuchumi na kuiona jamii kuona umuhimu wa kuwapa wanawake na watoto wa kike haki ya kushiriki katika shughuli za kiuchumi kama njia ya kuboresha maisha yao.
Hata hivyo wanawake wameushukuru uongozi wa Taasisi ya DadaHood Initiative kwa kuwapa nafasi wanawake wa mkoa wa Tabora kujifunza mambo mengi kutoka kwa wazungumzaji akiwemo Mkule ,Irene na na Bandora , nakieleza kuwa semina hiyo imewajengea ujasiri wa kufanya mabadiliko makubwa katika maisha yao.
Tamasha la The Orange Concert Imebeba kaulimbiu ya MWANAMKE NI CHAPA (BRAND) AMUA SASA limefanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani ambayo imeadhimishwa mwezi machi 8 mwaka 2025.
Wapili kutoka kulia ni mkurugenzi wa Taasisi ya DadaHood Initiative na mtangazaji maarufu kutoka Clouds FM, Mkuwe Issale (MAMYBABY), akitumia tamasha la The Orange Concert kutoa elimu kwa wanawake na wasichana mkoani Tabora.Mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi ya Salu Security Bandora Salum Mirambo akitoa elimu katika tamasha hilo .
0 Comments