Mhandisi James Jumbe Wiswa, mdau mkubwa wa michezo, ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni mbili kwa timu ya Stend United FC iwapo itaifunga timu ya Mtibwa Sugar FC ,katika mchezo utakao zikutanisha timu hizo na kupigwa Machi 17,2025 katika uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Machi 14, 2025,mkoani Shinyanga, Mdau wa michezo ,Jackline Isaro, amesema kuwa Motisha hiyo ime ahidiwa kutolewa na Mhandisi James Jumbe Wiswa kama sehemu ya juhudi za kuendeleza michezo mkoani Shinyanga na kuhakikisha timu ya Stend inafanya vizuri ili iweze kutoka hatua ya Champion Ship na kurejea Ligi kuu hali itakayo saidia kurejesha heshima ya timu ya Stand United FC 'Chama la Wana'.
Jackline amefafanua kuwa Mhandisi Jumbe, ambaye ni mkazi wa Shinyanga na mpenzi wa michezo, ameonyesha dhamira yake ya dhati kwa kuhamasisha wachezaji wa timu ya Stend united na mashabiki wa timu hiyo kwenda kuipa hamasa timu yao katika uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga Machi 17 .
Aidha, Jackline amesema kuwa Mhandisi James Jumbe ametangaza kununua tiketi miamoja kwa mashabiki wa timu ya Stand United FC ili waweze kuingia bure uwanjani huku zoezi la kutoa motisha kwa kila goli litakalofungwa na Stand United katika mchezo huo kwa kutoa shilingi 200,000 kwa kila goli likiwa endelevu.
"Mhandisi James Jumbe Wiswa ameichukulia kwa uzito mechi hii kati ya Stand United FC na Mtibwa Sugar FC, kwa kuwa yeye ni mkazi wa Shinyanga pia ni mwanamichezo kwamba endapo timu itashinda na kupata pointi tatu, atatoa zawadi ya shilingi milioni mbili . Pia motisha ya shilingi 200,000/= ambayo ameendelea kutoa kwa kila goli litakalofungwa na timu ipo pale pale," amesema Jackline.
Jackline amewahimiza wananchi wa mkoa wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu yao, Stand United FC ili iweze kupata pointi 3 muhimu katika uwanja wake wa nyumbani kwa kuibamiza timu ya Mtibwa Sugar.
"Tunataka kurudisha heshima ya mkoa wa Shinyanga kwa kuiinua timu hii inayodhaminiwa na Jambo Group kwa kuiwezesha timu ya Stend ," amesisitiza Jackline.
Kwa upande wake Afisa Habari wa timu ya Stand United FC, Ramadhani Zoro akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa motisha iliyo tolewa na Mhandisi Jumbe pamoja na jambo Group itachangia katika kushinda mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar FC.
"Tunamshukuru Mhandisi Jumbe kwa motisha hii kuahidi shilingi milioni 2 iwapo timu itashinda na tiketi 100 kwa mashabiki watakao ingia uwanjani bure si jambo dogo. Nasi tunaahidi kushinda mchezo huo , tumejiandaa vyema kwa mchezo huu na kikosi tayari kinaendelea na mazoezi ," amesema Zoro.Afisa Habari wa Stand United FC, Ramadhani Zoro akizungumza na waandishi wa habari
0 Comments