6/recent/ticker-posts

BENKI YA NMB YAENDESHA SEMINA KWA MAWAKALA WAKISHAPU ,MAGANZO NA SHINYANGA ,YA WAKUMBUSHA MAJUKUMU NA WAJIBU WAO

Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Manonga Gadiel Sawe akifungua semina kwa mawakala wabenki hiyo. 

 Na Amoj Media Shinyanga.

 Benki ya NMB imeendesha semina kwa mawakala wabenki hiyo kutoka Tawi la Kishapu,Maganzo  na Manonga Mkoani Shinyanga lengo ikiwa ni kuwakumbusha majukumu na wajibu wao wakati wakuwahudumia wateja wao.

 Semina hiyo ya siku moja imefanyika leo katika Ukumbi wa Makindo hall uliopo Manispaa ya Shinyanga mkoani humo na kuhusisha mawakala wote wabenki ya NMB kutoka Tawi la Kishapu ,Maganzo na Manonga. 

Akifungua semina hiyo Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Manonga Gadiel Sawe amesema lengo kuu la semina hiyo ni kutaka mawakala wafahamu na kuelewa mipango ya Benki ya Nmb iliyonayo katika kuhakikisha inawafikia na kuwahudumia mawakala wakiwa katika maeneo yao. 

Meneja wa huduma za mawakala kutoka benki ya NMB makao makuu Christine Mwidunda akitoa elimu kwa mawakala wa Benki ya NMB.

Kwa upande wake Meneja wa huduma za mawakala kutoka benki ya NMB makao makuu Christine Mwidunda akitoa elimu kwa mawakala amewasisitiza mawakala juu ya kutoa huduma bora kwa wateja kwa kufuata misingi na taratibu za kibenki pamoja na kuzingatia umuhimu na nafasi ya mteja katika maendeleo ya benki.

Aidha Christine amewakumbusha mawakala kuhusu nafasi yao katika kuinua uchumi wa Tanzania kwa kuungana na Benki Kuu ya Tanzania pamoja na serikali juu ya Vita ya kupambana na Utakatishaji wa fedha haramu.
"Tunaamini kuwa kupitia semina kama hizi, tutafanikiwa kuongeza ufanisi katika mawasiliano na kuhakikisha kwamba habari zinazohusu masuala ya fedha zinawafikia wananchi kwa usahihi.
Kwa upande wake meneja wabima kutoka Benki ya Nmb Kanda ya Magharibi Joseph Lawasare ametoa elimu kuhusu bima, mbalimbali ikiwemo Bima ya Faraja inayolenga zaidi kutoa mafao ya pole kwa mwananchi anapopatwa na changamoto ya msiba au ulemavu ambapo mteja anajiunga kwa Shilingi 200/= na anapata fao kuanzia Sh.milioni 1 hadi 6.

“Ndugu zangu hivi karibuni mmekuwa mkishuhudia majanga ya moto, mafuriko na ajali mbalimbali, hivyo ni vyema ukawa na bima ili unapopatwa na majanga usipate hasara na kuepuka kuyumba kiuchumi. Njoo ukate bima kwa ajili yako na mali zako. NMB inashirikiana na kampuni mbalimbali za utoaji bima”,amesema Joseph

Pia tunatoa elimu na ushauri kuhusu bima na kuuza bima ili kukabiliana na majanga yanapotokea., tunataka watu wote tuwafikie wapate bima ili kujikinga na hasara zitokanazo na majanga kwa kutoa fidia. Piatuna bima ya maisha, vyombo vya usafiri, bima kwa Wakulima na Wafugaji”,amesema Joseph
Mawakala wa Benki ya NMB wakiendelea kupatiwa semina.
Mawakala wa Benki ya NMB wakiendelea kupatiwa semina. 
Viongozi wa Benki ya NMB wakifatilia semina.

Meneja wa huduma za mawakala makao makuu Christine Mwidunda akitoa elimu kwa mawakala.

Post a Comment

0 Comments