KIKAO CHA UWT SHINYANGA CHA MPONGEZA RAIS SAMIA KWA UTENDAJI WAKE ,MWENYEKITI CCM MABALA APONGEZA MIKAKATI YA UWT KUTAFTA KURA ZA RAIS SAMIA 2025

Umoja wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Cha Mapinduzi (Ccm) Mkoa wa Shinyanga ukimkabidhi Mgeni Rasmi cheti cha pongezi katika kikao cha baraza la UWT mkoa.

Na Amoj Media Shinyanga

Umoja wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Cha Mapinduzi (Ccm) Mkoa wa Shinyanga umefanya Kikao cha wajumbe wake wa Kamati kwa Lengo la Kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan kwa utendaji wake na kupanga mikakati ya kuelekea uchaguzi mkuu wa Okitoba 2025 .

Akizungumza wakati wa kutoa Pongezi hizo mgeni rasmi katika kikao cha baraza hilo Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Mhe.Mabala Mlolwa amesema wanatambua mchango ambao unatolewa na Rais ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mama Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha umoja wa Wanawake Tanzania unakuwa imara, mshikamano na upendo wakati wote.

Mhe.Mlolwa ameongeza kuwa yeye kama Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga anatambua kazi kubwa iliyo fanywa na Rais Samia katika kipindi cha miaka minne hivyo ni vyema wanawake wakajipanga kutafta kura za Rais Samia itakapo fika wakati wa uchaguzi ili mkoa wa Shinyana uweze kushika nafasi yakwanza tofauti na uchaguzi uliopita ambapo mkoa ulishika nafasi ya pili kitaifa.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Bi. Gress Samwel amesema agenda Kuu ni kumpongeza Rais Samia kwa utendaji wake na jinsi anavyowahudumia Wananchi kwa ustadi na weledi mkubwa hasa kwa mambo makubwa ambayo ameyafanya kwa Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni pamoja na kiasi cha Fedha alichotoa kwa ajili ya shughuli za Maendeleo kwa kila Halmashauri ndani ya miaka minne aliyo kaa madarakani pamoja na kupanga mikakati ya kupata kura za Rais Samia katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Bi. Gress ameongeza kuwa Mama Samia ameweza kumtua Mwanamke ndoo kichwani kwa kuongeza upatikanaji kwa urahisi wa Maji katika Mkoa wa Shinyanga.

Aidha ameongeza kuwa Mhe. Samia ameweza kufanikisha Ujenzi wa Shule za Msingi, Sekondari,Vyuo na Vyuo vya ufundi stadi(Veta) ambapo Itasaidia kuhakikisha kila mtoto wa kitanzania anapata elimu iliyo bora .

Rais Samia ameweza kufanya uteuzi wa nafasi mbalimbali za wanawake katika nafasi nyeti na za juu huku akiwataka wanawake wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wakati wa uchaguzi mkuu.

Naye Katibu wa Umoja wa Wanawake Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Bi. Habiba Ismail amesema Baraza na Jumuiya ya Wanawake wa Ccm Taifa na Mikoa yote wanaungana na Mwenyekiti wao Kitaifa katika kutambua mchango mkubwa unaotolewa katika kuiletea Tanzania Maendeleo kuanzia kwa Wananchi wake na Kulitangaza Taifa kiujumla.

Kwa upande wao baadhi ya wabunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Christina Mzava na Santiel Kilumba wakitoa salamu katika kikao hicho cha baraza wameahidi kuungana kwa pamoja katika kuelezea miradi ya maendeleo iliyo tekelezwa na Rais Samia kwa wananchi pamoja na kutafta kura za Rais Samia itakapo fika wakati wa uchaguzi ikiwa ni sehemu ya Shukrani kwa Rais Samia juu ya mambo mazuri aliyo yafanya katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mkoa wa Shinyanga.

Umoja wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Cha Mapinduzi (Ccm) Mkoa wa Shinyanga wakiwa nje ya ukumbi wakisubili kumpokea Mgeni Rasmi kwa ajili ya katika kikao cha baraza la UWT mkoa.Umoja wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Cha Mapinduzi (Ccm) Mkoa wa Shinyanga ukimkaribisha Mgeni Rasmi katika kikao cha baraza la UWT mkoa.
Umoja wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Cha Mapinduzi (Ccm) Mkoa wa Shinyanga wakiendelea na kikao
cha baraza la UWT mkoa.
Katikati ni Mhe.Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Christina Mzava akijiandaa kushiriki kikao cha baraza la UWT mkoa.
Kamati ya uchumi ya Umoja wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Cha Mapinduzi (Ccm) Mkoa wa Shinyanga katika kikao cha baraza la UWT mkoa.
Kamati ya uchumi ya Umoja wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Cha Mapinduzi (Ccm) Mkoa wa Shinyanga katika kikao cha baraza la UWT mkoa.
Umoja wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Cha Mapinduzi (Ccm) Mkoa wa Shinyanga wakiwa nje ya ukumbi wakisubili kumpokea Mgeni Rasmi kwa ajili ya katika kikao cha baraza la UWT mkoa.
Umoja wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Cha Mapinduzi (Ccm) Mkoa wa Shinyanga wakiwa nje ya ukumbi wakisubili kumpokea Mgeni Rasmi kwa ajili ya katika kikao cha baraza la UWT mkoa.
 Mhe.Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Christina Mzava akitoa salamu zake kwa wajumbe walio shiriki kikao cha baraza la UWT mkoa.
Mhe.Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Christina Mzava akitoa salamu zake kwa wajumbe walio shiriki kikao cha baraza la UWT mkoa.
Mhe.Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Santiel Kilumba akitoa salamu zake kwa wajumbe walio shiriki kikao cha baraza la UWT mkoa.
Kushoto ni Mhe.Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Santiel Kirumba akiwa katika kikao cha baraza la UWT mkoa.
Mhe.Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Santiel Kilumba akishiriki kikao cha baraza la UWT mkoa.
Umoja wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Cha Mapinduzi (Ccm) Mkoa wa Shinyanga ukimkabidhi Mgeni Rasmi zawadi katika kikao cha baraza la UWT mkoa.
Umoja wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Cha Mapinduzi (Ccm) Mkoa wa Shinyanga ukimkabidhi Mgeni Rasmi zawadi katika kikao cha baraza la UWT mkoa.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Bi. Gress Samwel akizungumza na wajumbe wa kikao cha baraza UWT mkoa.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Bi. Gress Samwel akizungumza na wajumbe wa kikao cha baraza UWT mkoa.

TAZAMA PICHA MATUKIO YA KIKAO CHA BARAZA UWT KIKIENDELEA.

Post a Comment

0 Comments