Na Mwandishi wetu Amoj Media Shinyanga.
Machi 22, 2025, Mbunge wa Jimbo la Solwa, Mhe. Ahmed Ally Salum ameendelea na ziara yake katika Kata ya Usanda, Kijiji cha Nzagaluba, kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Moja ya miradi aliyoikagua ni ujenzi wa mabweni mawili yanayogharimu kiasi cha Shilingi.milioni 272,000,000/=, ambapo kwa sasa mradi huo upo katika hatua ya upauaji pia amekagua ujenzi wa Shule ya Msingi Singita, ambao umefadhiliwa na Serikali Kuu kwa kiasi cha Shilingi milioni 27,000,000/= ambayo ujenzi wake umefikia hatua ya usafishaji wa eneo na kuletwa kwa vifaa vya ujenzi.
Katika Kijiji cha Singida, Mhe. Ahmed Ally Salum amekagua mradi wa ujenzi wa zahanati ambao unatarajiwa kukamilika kwa gharama ya Shilingi milioni 25,079,019/=huku Katika Kijiji cha Manyada, Mhe. Mbunge akikagua maendeleo ya ujenzi wa zahanati inayo jengwa kwa kiasi cha shilingi milioni 16,000,000,/= fedha ambazo ni michango ya wananchi.
Baada ya kumaliza ziara yake katika Kata ya Usanda, Mhe. Ahmed Ally Salum amefanya ziara katika Kata ya Masengwa na kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Shule ya Sekondari Masengwa yenye thamani ya takribani Shilingi milioni 74,000,000/= shule ambayo Mbunge pia amefanikisha kupeleka nishati ya umeme katika shule hiyo na vijiji vilivyopo katika kata ya Masengwa.
Aidha Mhe.Ahmed emesema kuwa Kata ya Masengwa imepokea shilingi milioni. 140,000,000/= kwa ajili ya ukarabati wa miundo mbinu ya barabara na kusimamia uchimbaji wa kisima kirefu pamoja na upembuzi yakinifu wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria utakao sambazwa hadi Kijiji cha Ikonda.
Mhe. Ahmed amepongeza juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kupeleka fedha za maendeleo katika Jimbo la Solwa huku Wananchi wa Jimbo la Solwa wakieleza kufurahishwa na juhudi hizo na kuahidi kumpatia kura wakati wa uchaguzi kama sehemu ya shukrani.
Katika ziara yake, Mhe. Mbunge amepokea wanachama wapya wanne kutoka vyama vya CUF na CHADEMA.ambapo Wanachama wameeleza sababu ya kujiunga na CCM kuwa nibaada ya kutazama utekelezaji wa Ilani ya chama hicho kwa vitendo.
Wananchi wakiwasilisha changamoto zao kwa Mhe.Mbunge wa jimbo la Solwa Mhe.Ahmed kwenye mkutano.

Wananchi wakimsikiliza Mhe.Mbunge wa jimbo la Solwa Mhe.Ahmed kwenye mkutano.
Wananchi wakimsikiliza Mhe.Mbunge wa jimbo la Solwa Mhe.Ahmed kwenye mkutano. Wananchi wakiwasilisha changamoto zao kwa Mhe.Mbunge wa jimbo la Solwa kwenye mkutano wa mbunge



TAZAMA PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA ZIARA YA MHE.AHMED JIMBO LA SOLWA.
TA


0 Comments