
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya
Mwakitolyo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani humo kimemtunuku cheti cha
pongezi Mbunge wa Jimbo la Solwa, Mhe. Ahmed Ally Salum, kutokana na juhudi
zake kubwa katika kupigania maendeleo ya wananchi wa kata hiyo na jimbo la
Solwa kwa ujumla.
Zoezi la kumkabidhi cheti cha pongezi
Mhe.Mbunge limefanyika Machi 21,2025, katika kata hiyo, wakati wa ziara ya Mhe.
Ahmed Ally Salum ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kusikiliza
kero zinazo wakabili wananchi wa kata hiyo.
Katika ziara hiyo Mhe.Ahmed ametembelea
kijiji cha Nyang'ombe na kukagua ujenzi wa zahanati yenye thamani ya shilingi
91,600,000/=ambayo imejengwa kupitia ufadhili wa wadau mbalimbali na serikali
na kuaahidi kutoa shilingi 2,000,000/= kwa ajili ya kukamilisha mfumo wa maji
katika zahanati hiyo ili kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa
wagonjwa na wahudumu wa afya wanao fanya kazi katika zahanati.
Aidha Mhe. Ahmed amewashukuru wadau
waliochangia ujenzi wa zahanati hiyo, akisema kuwa imesaidia kupunguza adha ya
wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za matibabu. na kuwaomba wadau
kuendelea na moyo huo wa kujitolea katika kuchangia miradi ya maendeleo.
Pia, Mhe. Ahmed alifanya ziara
katika Kata ya Solwa, Kijiji cha Manheigana, na kukagua maendeleo ya ujenzi wa
Shule ya Sekondari ya Manheigana. Aliahidi kuchangia mifuko 100 ya saruji kwa
ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ili kupunguza msongamano wa
wanafunzi katika shule hiyo. Aidha, alitoa mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya
ujenzi wa chumba cha kujifungulia akina mama katika Kata ya Solwa, ikiwa ni
sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha
miundombinu ya sekta ya afya nchini.Wananchi wakimshangilia mbunge wa Jimbo la Solwa, Mhe. Ahmed Ally Salum alipowasili katika kata hiyo kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi.


Wananchi wakimsikiliza mbunge wa Jimbo la Solwa, Mhe. Ahmed Ally Salum wakati akisikiliza kero za wananchi.
TAZAMA
PICHA MATUKIO YA ZIARA YA MBUNGE WA JIMBO LA SOLWA, MHE. AHMED
IKIENDELEA .
0 Comments