6/recent/ticker-posts

ATAWAS YABISHA HODI KANDA YA ZIWA KUTAFTA TIMU ZITAKAZO SHIRIKI LIGI YA MAJI CUP NGAZI YA TAIFA MKOANI TANGA,KASHWASA YAICHAPA 4 KWA 3 SHUWASA



LIGI YA MAJI CUP 2025 YAANZA KUTIMUA VUMBI CCM KAMBARAGE

Chanzo Shinyanga Press club Blog

Ligi ya Maji CUP 2025 Kanda ya Ziwa, imeanza kutimua vumbi katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga,ikishirikisha Timu kutoka Mamlaka za Maji.


Costantino Chiwaligo.

Ligi hiyo imeanza leo Mei 31,2025, ambayo imeandaliwa na Taasisi ya watoa huduma za Maji nchini ATAWAS, ambapo katika mashindano hayo Timu 3 bora zitakwenda kushiriki michuano ya kitaifa ya Mamlaka za Maji Jijini Tanga.

Mtendaji Mkuu wa ATAWAS Costantino Chiwaligo, ambaye ndiye mratibu wa mashindano hayo,amesema ligi hiyo inashirikisha Timu za Mamlaka za Maji kutoka Kanda 8, ambapo kwa sasa wapo katika Kanda ya Ziwa.


“Lengo la Mashindano haya ni kuangazia mafanikio ya sekta ya maji chini ya utawala wa awamu ya sita,”amesema Costantino.

Aidha, amesema katika mashindao hayo, ambapo unachezwa mpira wa miguu na pete, pia wameshirikisha baadhi ya timu za jamii,ili kuweza kufikisha ujumbe kwa wananchi, kwa wao kuwa mabalozi wazuri wa kuzuia uharibifu wa vyanzo vya maji,miundombinu na utunzaji wa mazingira.


Nao baadhi ya washiriki wa michezo hiyo kutoka Mamlaka za maji,wamesema ligi hiyo licha ya kuonyesha vipaji vyao na kuimarisha afya,itasaidia pia kufikisha ujumbe kwa jamii juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji, pamoja na kutoa taarifa pale wanapoona kuna maji yanavuja,ili kuzuia upotevu wa maji.

Katika Mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo Kati ya Kashwasa na Shuwasa, ambapo Kashwasa waliondoka na ushindi wa Magoli 4-3.



















Post a Comment

0 Comments