Mabula J. Magangila
Chanzo – Malunde Blog
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekamilisha zoezi la kura za maoni kwa ajili ya kuwapata wagombea wa nafasi ya Ubunge katika Majimbo ya Kahama Mjini, Msalala na Ushetu mkoani Shinyanga, ambapo wanachama wake walijitokeza kwa wingi kuwachagua wawakilishi wao kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Akitangaza matokeo hayo,Katibu wa CCM Wilaya ya Kahama, Andrew Chatwanga,amesema katika Jimbo la Msalala, jumla ya kura 7,845 zilipigwa,ambapo kura halali ni 7,685 na zilizoharibika ni 160 ambapo Mabula J.Magangila ameongoza kwa kura 5,518, akifuatiwa na Ambrose N.Nakale kura aliyepata kura 929, Ezekiel Maige aliye pata kura 791,Simon James Lufega aliye pata kura 189, Edson Simba Masondole aliye pata kura 152 na Ramadhani Shiganza aliye pata kura 105
Wakati huo huo, CCM Wilaya ya Kahama imemtangaza Emmanuel Peter Cherehani kuongoza katika matokeo ya awali ya kura za maoni Jimbo la Ushetu, huku matokeo ya mwisho yakisubiriwa kutokana na marudio ya uchaguzi katika kata tatu; Ubagwe, Mapamba na Bulungwa kufuatia malalamiko ya baadhi ya wanachama.
Katibu wa CCM Wilaya ya Kahama, Andrew Chatwanga, amewataka wanachama na wagombea wote kuwa watulivu na kusubiri maamuzi ya mwisho ya vikao vya chama kwa nidhamu na ustaarabu, kulingana na maadili ya CCM.

0 Comments