6/recent/ticker-posts

MKURUGENZI SALU SECURITY BANDORA SALUMU MIRAMBO ASHINDA KURA ZA MAONI CCM KATA YA CHEMCHEM KWA KISHINDO - TABORA

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Salu Security, Bandora Salumu Mirambo, ameibuka mshindi CCM kugombea nafasi ya Udiwani katika Kata ya Chemchem, Manispaa ya Tabora.

Na Mwandishi Wetu Amo Blog Tabora.

Mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chemchem, Manispaa ya Tabora.
, umefikia tamati ambapo Bandora Salumu Mirambo ameibuka mshindi kwa kishindo baada ya kupata kura 83 kati ya kura 161 zilizopigwa.

Katika kinyang'anyiro hicho, Suleiman Adallah Omar ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 77, akifuatiwa na Neema Alex Kasanji aliyepata kura 1.

Akitangaza matokeo hayo, msimamizi wa uchaguzi huo, Jah Kaducha , amewataka wanachama wa CCM kuendelea kudumisha mshikamano wa chama licha ya tofauti za matokeo.

“Kwakuwa huu ni mchakato wa awali hivyo, wale ambao kura zao hazikutosha, waendelee kushirikiana na mshindi kwa manufaa ya chama chetu kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.”

Post a Comment

0 Comments