Chanzao- Malunde 1 blog
Hatimaye mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Mjini, Shinyanga, umefikia tamati ambapo Salum Kitumbo ameibuka mshindi kwa kishindo baada ya kupata kura 47 kati ya kura 126 zilizopigwa.
Katika kinyang'anyiro hicho, Abdulaziz Sakala ambaye ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 37, akifuatiwa na Abubakar Mukadam aliyepata kura 34. Wengine ni Nasoro Warioba aliyepata kura 4 na Rahma Kware aliyepata kura 2, huku kura 2 zikiharibika.

Akitangaza matokeo hayo, msimamizi wa uchaguzi huo, Mwalimu Burugu, amewataka wanachama wa CCM kuendelea kudumisha mshikamano na mshikamano wa chama licha ya tofauti za matokeo, akisema kuwa:
“Huu ni mchakato wa ndani wa awali. Hivyo, wale ambao kura zao hazikutosha, waendelee kushirikiana na mshindi kwa manufaa ya chama chetu kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.”
Salum Kitumbo ni kada wa muda mrefu wa CCM, aliyejiunga na chama hicho tangu mwaka 1984. Ana elimu ya Shahada ya Kwanza ya Biashara na Utawala kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama.

Mbali na siasa, Kitumbo ni mshauri wa kibiashara katika makampuni ya Jambo Group na anatajwa kuwa na ushawishi mkubwa katika kuimarisha mshikamano wa chama hususan katika Kata ya Mjini.

0 Comments