6/recent/ticker-posts

FLAVIANA MATATA AKABIDHI MATUNDU 24 YA VYOO SHULE YA SEKONDARI MAZINGE DC SAMIZI ,ASEMA WATAKAO HARIBU MIUNDOMBINU KUKIONA CHA MOTO .


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Foundation, Flaviana Matata kwenye hafla ya kukabidhi matundu 24 ya vyoo shule ya Sekondari Mazinge.


Na Marco Maduhu,SHINYANGA



TAASISI ya Flaviana Foundation imekabidhi matundu ya vyoo 24 na chumba maalumu cha kujistili hedhi katika Shule ya Sekondari Mazinge iliyopo Manispaa ya Shinyanga, na kuwaondolea adha wanafunzi kujisaidia kwa Foleni.

Makabidhiano hayo ya matundu ya vyoo na chumba maalumu cha kujistili hedhi yamefanyika leo Juni 1,2023 katika Shule hiyo ya Sekondari Mazinge, huku Mgeni Rasmi akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Foundation, Flaviana Matata, akizungumza wakati wa kukabidhi matundu hayo vyoo, amesema aliguswa na shule hiyo ya Sekondari Mazinge kukabiliwa na upungufu mkubwa wa matundu ya vyoo, na kulazimika wanafunzi kujisaidia kwa foleni, huku watoto wa kike wakiwa hawana chumba maalumu cha kujistili na hedhi.

“Nawaomba wanafunzi miundombinu hii ya vyoo muitunze na muwe wasafi, na msome kwa bidii na kutimiza ndoto zenu, na wanafunzi wa kike msiwe watoro shuleni sababu ya kuwa katika siku zenu, vyumba vya kujistili na hedhi tumewajenga katika vyoo hivi ambavyo tumekabidhi leo,”amesema Flaviana.

Naye Meneja Miradi kutoka Taasisi hiyo ya Flaviana Foundation Lineth Masala, amesema ujenzi huo wa mtundu ya vyoo 24 katika Shule hiyo ya Sekondari Mazinge, ulianza Rasmi March Mwaka huu na kukamilika june kwa gharama ya Sh.milioni 58 kupitia ufadhili wa Diamonds do Good.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi, ameipongeza Taasisi hiyo ya Flaviana Foundation kwa kuiunga Mkono Serikali kutatua matatizo mbalimbali katika Sekta ya Elimu, na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano, huku akiwataka wanafunzi wavitumie vyoo hivyo kwa matumizi sahihi na siyo kuharibu miundombinu yake.

Mkuu wa shule ya Sekondari Mazinge James Msimba, amesema awali shule hiyo walikuwa wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa mtundu ya vyoo, ambapo walikuwa na matundu Sita, matundu Manne (4)yanatumiwa na wanafunzi wa kike 507, na mawili (2) wanafunzi wa kiume 494, hivyo kupata matundu hayo 24 yatapunguza upungufu uliokuwepo awali na shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1,001.

Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo akiwamo Mary Maximilian, amesema upatikanaji wa mtundu hayo ya vyoo 24, ambayo 12 ya wanafunzi wa kike, na 12 kiume, yatawasaidia kuondokana na usumbufu wa kujisaidia kwa foleni, pamoja na kupata vyumba maalumu vya kujistili na hedhi.


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga he.Johari Samizi akizungumza kwenye hafla ya kukabidhiwa matundu 24 ya vyoo na chumba maalumu cha kujistili hedhi katika Shule ya Sekondari Mazinge iliyopo Manispaa ya Shinyanga kutoka Taasisi ya Flaviana Matata.



Maofisa kutoka Taasisi ya Flaviana Matata Foundation wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi matundu 24 vya vyoo na chumba maalumu cha kujistili hedhi katika shule ya Sekondari ya Mazinge .






 Flaviana Matata akiwa katika hafla ya kukabidhi matundu 24 ya vyoo Shule ya Sekondari ya Mazinge .



Mkurugenzi wa Flaviana Foundation, Flaviana Matata akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi matundu 24 ya vyoo .




Mkurugenzi wa Flaviana Foundation, Flaviana Matata akizungumza na wanafunzi kwenye hafla ya kukabidhi matundu 24 ya vyoo .





Viongozi meza kuu wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi matundu 24 ya vyoo na chumba maalumu cha kujistili hedhi.




Viongozi meza kuu wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi matundu 24 ya vyoo na chumba maalumu cha kujistili hedhi  shule ya Sekondari Mazinge .



Mkuu wa shule ya Sekondari Mazinge James Msimba akisoma taarifa ya shule.






Mkurugenzi wa Flaviana Foundation, Flaviana Matata akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi matundu 24 ya vyoo .




Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura  akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi matundu 24 vya vyoo  shule ya Sekondari Mazinge.




Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi matundu 24 ya vyoo na  Shule ya Sekondari Mazinge .




wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi matundu 24 vya vyoo na chumba maalumu cha kujistili hedhi katika shule ya Sekondari ya Mazinge .


Post a Comment

0 Comments