Shirika
lisilo la Kiserikali linatoa msaada wa Kisheria Mhola limetoa elimu ya
kushiriki kwenye fulsa za uongozi kwa kina mama
Wilayani Muleba Mkoani Kagera ambao utawasaidia kushiriki kwenye vikao
vya maamuzi pamoja na kuonesha uwezo wao wa uongozi.
Akifungua
mafunzo hayo mkurugenzi wa Shirika la Mhola Bwana Saulo Marauli amesema mafunzo
hayo yanahusisha Wanawake Viongozi wa
Serikali za vijiji kutoka Kata za Katoke, Izigo na Muhutwe ambayo yatafanyika
kwa muda siku mbili kwenye ukumbi wa makao makuu ya shirika hilo Wilayani
Muleba.
Bwana
Marauli amesema kuwa bado kwenye jamii kuna changamoto ya baadhi ya wakina mama
kushindwa kujiuhusisha na shughuli za kiuchumi ikiwemo kufuga na kulima badala
yake wanakuwa tegemezi kwenye jamii hivyo mafunzo hayo yatawasaidia wakina mama
kujua haki zao ikiwemo sheria, uchumi na afya zao.
Wakili Raymond Laurent kutoka Shirika la Mhola
amewataka wakina mama kuwa na mawazo chanya ambayo yatawasaidia kujitokeza
kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwa lengo la kujikwamua kiuchumi badala
ya kubaki kuwa tegemezi kwenye jamii.
Wakili
Laurent amesema kuwa wanawake viongozi wanaowajibu wa kuhakikisha wanakuwa
mfano bora wa kuigwa kwenye jamii ikiwemo kuondoa upendeleo, kusuruhisha,
kuacha alama na kuinua kiwango cha utendaji kazi kwa lengo la kuendelea
kuaminiwa na jamii.
Aneth
John ni Mtendaji wa Kijiji cha Kimbugu na Alikanjera Audax ni mwenyekiti wa
Kitongoji cha Bulimba wamesema kuwa bado wakina mama wamekuwa na changamoto ya
kunyanganywa mali zao ikiwemo mashamba na nyumba na kubaki tegemezi baada ya
kukopeshwa na taasisi za kifedha na kushindwa kurejesha kutokana na uhaba wa
elimu ya matumizi sahihi ya fedha hivyo kuna haja ya kupatiwa elimu ili kuondoa
changamoto hiyo.
Aidha
shirika hilo la Mhola linatarajia kutoa mafunzo kwa Wanawake Viongozi kwa mwaka
2023 kwenye Kata ambazo ni Izigo, Kasharunga, Katoke, Muhutwe, Mubunda, Kagoma,
Bureza na Gwanseri na Kijiji cha Kyamworwa lengo ni kuhakikisha wakina mama hao
wanatumia fulsa za kiuchumi zilizopo kwenye maeneo yao.
Wakili Raymond Laurian akitoa elimu ya uongozi kwa washiriki wa semina hiyo
WaShiriki wakisikiliza kwa mada mbalimbali zinazofundishwa kutoka kwa wawezeshaji.
Mtendaji wa Kijiji Cha Kimbugu akichangia mawazo juu ya mada ya wanawake na uongozi
0 Comments