6/recent/ticker-posts

KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI YAPONGEZA THPS KWA UTOAJI WA HUDUMA BORA HUDUMA ZA KUDHIBITI UKIMWI SHINYANGA, NICODEMAS ASISITIZA USHIRIKISHWAJI


Mwenyekiti wa kamati ya kudhibiti ukimwi wilaya ya Shinyanga Nicodemas Simon akisaini kitabu cha wageni kituo cha afya Nindo.

Na AMO BLOG SHINYANGA.

Kamati shirikishi ya kudhibiti ukimwi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga ikiongozwa na mwenyekiti wa kamati hiyo  Nicodemas Simon amelipongeza Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa kutoa msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo gari moja na kuajili watumishi saba wamda katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani humo ikiwa ni sehemu ya kuboresha usimamizi wa Huduma za Afya ndani ya halmashauri hiyo ikiwemo kuongeza kiwango cha utoaji wa Huduma za UKIMWI na Matunzo kwa Watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.
Akizungumza na watumishi pamoja na viongozi wa THPS mwenyekiti wa kamati ya kudhibiti Ukimwi katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nicodemas Simon ameeleza lengo lakufanya ziara katika kituo cha afya Nindo nikutaka kuona shughuli zinazo tekelezwa na THPS katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga nikutaka kuona Shirika hilo linavyo shirika katika  mapambano ya VVU na Ukimwi ndani ya  halmashauri hiyo pamoja na kupata taarifa ya Shughuli mbalimbali zinazo fanywa na THPS katika halmasghauri ya shinyanga.
“Tunawashukuru sana THPS chukua maua yenu maana kazi mnayo fanya nikubwa sana maana tumeona mmetusaidia kuajili watumishi 7 wamda ambao wanafanya kazi nzuri katika halmashauri yetu katika  kuhakikisha huduma za afya zinawafikia wananchi kama ilivyokusudiwa hususani katika mapambano ya VVU na Ukimwi , Naomba THPS Tuendelee kushirikiana na serikali katika kupambana na maambukizi ya VVU na Ukimwi ili halimashauri yetu itoke kwenye nafasi ya kuwa na kiwango cha maambukizi ya Asilimia 1.2 na hatimaye tufikie Asilimia 0,amesema Nicodemas.

Ametumia fursa hiyo kuwahamasisha wadau wengine kujitokeza na kuunga mkono jitihada zinazo fanywa na halmashauri katika mapambano ya VVU na Ukimwi pamoja na afua nyingine maana halmashauri hiyo kupitia mkurugezi wake na madiwani wanatoa ushirikiano wakutosha kwa wadau wanao fika katika halmashauri ya Shinyanga na kuonyesha nia ya kushirikiana na halmashauri katika kuchochea maendeleo.

Aidha Nicodemas ameongeza kuwa  THPS imeongeza kiwango cha utoaji chanjo ya UVIKO -19 kwa jamii pamoja na utoaji wa huduma za UKIMWI na matunzo kwa watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

Akitoa ufafanuzi wa baadhi ya shughuli walizo fanya katika kituo cha afya Nindo  Meneja wa  Shirika la THPS, Dkt.Amos Scott amesema THPS ambayo inajihusisha na huduma za maambukizi ya VVU na UKIMWI na Matunzo kwa watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI imetoa gari moja na kuajili watumishi 7 wamda katika halmashauri hiyo ili kuboresha  Huduma za VVU na UKIMWI ndani ya halmasgauriya wilaya ya Shinyanga na kupunguza kiwango cha maambukizi .

“THPS hivi sasa inafanya kazi katika halmashsauri ya wilaya ya  shinyanga na halmashauri nyingine kwa lengo la kuongeza nguvu katika masuala ya VVU na UKIMWI pamoja na utoaji chanjo ya UVIKO – 19”,amesema Scott.

Katika hatua nyingine amesema THPS inatekeleza miradi ya VVU na UKIMWI na UVIKO – 19 katika halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga  na maeneo mengine nchini ikiwa nisehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali katika mapambano ya VVU na Ukimwi.

Kwa upande wake, mkuu wa kitengo cha Tiba na Matunzo Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Erasto Gabriel ameishukuru THPS kwa kuimarisha, ushirikiano na halmashauri ya Shinyanga hususani katika kuongeza nguvu katika mapambano ya kudhibiti maambukizi ya VVU na Ukimwi katika halmashauri hiyo maana kwasasa wamefanikiwa kuyafikia makundi hatarishi na kufanya shughuli mbalimbali za upimaji ikiwa ni pamoja na kuwapaelimu ya kujikinga na maambukizi ya VVU na Ukimwi hali itakayo saidia kuendelea kupunguza kiwango cha maambukizi ndani ya halmashauri hiyo.

Mwenyekiti wa kamati ya kudhibiti ukimwi wilaya ya Shinyanga Nicodemas Simon akiangalia baadhi ya vifaa vilivyo tolewa na THPS.


Meneja THPS mkoa wa Shinyanga Dkt.Amos Scott akitoa taarifa ya utendaji kazi wa shirika katika kituo cha afya Nindo. 


Meneja THPS mkoa wa Shinyanga Dkt.Amos Scott pembeni akisaini kitabu cha wageni.baada ya kutembelea kituo cha afya Nindo. 


Kaimu mratibu wakifua kikuu na ukoma wilaya ya Shinyanga Dkt.Damas Nyansira akieleza msaada ulio tolewa na THPS kwa wajumbe wa kamati ya kudhibiti ukimwi.
  

Mkuu wakitengo cha Tiba na Mtaunzo Halmashauriya wilaya ya Shinyanga Erasto Gaabriel akitoa taarifa ya hali ya maambukizi ya VVU na Ukimwi ndani ya halmashauri hiyo.


Kamati ya kudhibiti ukimwi ikifatilia taarifa inayo tolewa na mkuu wakitengo cha Tiba na Mtatun
zo kituo cha afya Nindo.


Meneja THPS Mkoa wa Shinyanga Dkt.Amos SCOTT akitoa taarifa ya utendaji kazi wa THPS katika kituo cha afya Nindo.



Mabinti balehe wanao wezeshwa na THPS wakipatiwa mafunzo ya kujikinga na maambukizi ya VVU na ukimwi kituo cha afya Nindo.

Mwenyekiti wa kamati ya kudhibiti ukimwi wilaya ya Shinyanga Nicodemas Simon akiangalia baadhi ya vifaa vilivyo tolewa na THPS.


Baadhiya msaada wa vifaa vilivyo tolewa na THPS katika kituo cha afya Nindo.

Wajumbe wa kamati ya kudhibiti ukimwi wilaya ya Shinyanga wakiwa kituo cha afya Nindo  wakisikiliza maelekezo ya wataalamu katika kituo hicho.

Post a Comment

0 Comments