Serikali
mkoani Shinyanga imeuagiza uongozi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga mkoani humo kuhakikisha wanaongeza juhudi za
ukusanyaji mapato ili waweze kufikia malengo waliyo jiwekea ya kukusanya mapato
kwa asilimia 100 .
Maagizo
hayo yametolewa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe.Christina Mndeme kwenye kikao
maalum cha Baraza la Madiwani walicho keti kwa ajili ya kupokea ,kupitia na
kujadili hoja ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG
Mndeme amebainisha
kuwa kuanzia mwezi Julai 2022 hadi Juni 19, 2023 wamefikia asilimia 75 ya
ukusanyaji wa mapato na kueleza kuwa kisi cha asilimia 25 bado kinahitajika ili
kufikia malengo waliyojiwekea katika ukusanyaji mapato kwa mwaka.
Aidha Mndeme
ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa kupata hati safi huku
akiwasii kudumisha umoja namshikamano baina ya wataalamu na madiwani hali
itakayo saidia kuongeza kiwango cha ukusanyaji wamapato na kuchochea maendeleo
ya halmashauri hiyo.
Halmashauri
hii inatakiwa isimamie sheria,kanuni na miongozo kwani nafahamu mnaweza maana
mnayo timu nzuri ya wataalamu na madiwani ambao wamesababisha halmashauri kupata
hati safi” amesema Mndeme.
Awali
mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Simon Barege akizungumza
katika kikao hicho ameahidi kutoa ushirikiano kwa madiwani na kutumia maarifa
aliyo nayo kuchochea maendeleo ya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Naye Mkaguzi
Mkuu wa Hsabau za Serikali Mkoa wa Shinyanga, Patrick Lugisi ameshauri kamati
ya fedha kuandaa taarifa za muhtasari wa kikao vizuri ili kurahisisha kazi kwa
wakaguzi na kufanikiwa kujibu hoja.
“Halmashauri
hii inahoja 56 ambazo bado hazijajibiwa zinatakiwa kufanyiwa kazi ili isibaki
hata hoja moja , amesema Lugisi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje ameahidi kushirikiana na madiwanipamoja na wataalamu kutekeleza maagizo yaliyo tolewa na mkuu wa mkoa.
Mambo ya ufunguzi wa kikao cha baraza maalumu la madiwani yanaendelea.
Maombi yanaendelea.
mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Simon Barege akizungumza katika baraza maalumu la madiwani.
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Prf.Siza Tumbo akiwa kwenye kikao cha baraza maalumu la madiwani.
0 Comments