6/recent/ticker-posts

VYUMBA 7 VYA JJ VINAVYO MILIKIWA NA UWT CCM SHINYANGA VYATEKETEA KWA MOTO 6 VYA OKOLEWA NA ZIMAMOTO .



Kamanda wa jeshi la zimamoto  na uokoaji mkoa wa Shinyanga Martin Nyambala.

NA AMO BLOG SHINYANGA.

Maduka 7 kati ya 13 ya Wafanyabiashara walio panga katika jengo la Umoja wa Wanawake Tanzania UWT mkoa wa Shinyanga, maarufu kama JJ yaliyopo mkabala na ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Shinyanga yameteketea kwa moto huku maduka 6 ya kiokolea na jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani humo.

Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wajeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Shinyanga Martin Nyambala amesema kuwa wamepokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa wafanyabiashara na kueleza kuwa wamefanikiwa kufika eneo la tukio kwa wakati na kufanikiwa kuzima moto huo ambapo jumla ya vyumba 6 vimeokolewa baada ya jitihada za jeshi hilo na wafanya biashara.

 

Aidha kamanda Nyambala amewataka wananchi kutoa taarifa za majanga yamoto kwa wakati huku akeeleza kuwa bado wanaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo .

 Kwa upande wake Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga Asha Kitandala, amesema kuwa amepokea taarifa zatukio hilo kwa masikitiko makubwa maana tukio hilo limewarudhisha nyuma kimaendeleo na kueleza kuwa Wafanyabishara waliokuwa wakifanyia biashara katika jengo hilo wamepata hasara kutokana na bidhaa zao kuteketea kwa moto.


Wakielezea tukio hilo baadhi ya wafanyabishara ambao malizao zimeteketea kwa moto wamesema wamepigiwa simu usiku na walinzi wanao linda vibanda vyao wakiwajulishwa kuhusu maduka yao kuteketea kwa moto.

 


vitu vilivyo teketea kwa moto.





Baadhi ya wafanyabiashara wakitazama bidhaa zao zilizo teketea kwa moto.




Kamanda wa jeshi la zimamoto  na uokoaji mkoa wa Shinyanga Martin Nyambala.







 

Post a Comment

0 Comments