Wahitimu wa darasa la awali SAPPS wakikabidhiwa vyeti na mgeni rasimi.
Wahitimu
wa Awali wanao soma Shule ya Shinyanga Adventist Pre and Primary School (SAPPS)
Inayo milikiwa na Nyanza Gold Belt Field (NGBF) yenye usajili wanamba
EM18166 wamehitimu mafunzo yao ya awali ikiwa ni mandalizi ya kujiunga na
masomo ya darasa la kwanza mwaka 2024.
Akizungumza
na wazazi na walezi wawatoto walio hitimu mgeni rasmi katika mahafali hayo
Kiliani Wembe amewataka kuwaandikisha elimu ya msingi watoto wote waliohitimu
elimu ya awali ili waweze kuanza darasa la kweanza mwakani.
Pia
Wembe ametoa kiasi cha shilingi laki tano ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono
juhudi za shule hiyo katika kuboresha miundo mbinu ya shule hiyo huku akiahidi
kulipa gharama za fomu kwa wazazi na walezi watakao jitiokeza kuandikisha
watoto wa nao anza darasa la awali mwaka 2024.
Aidha
wembe ameipongeza shule hiyo kwa kufanya vizuri kitaaluma ikiwemo kusisitiza
nidhamu na maadili kwa wanafunzi wanao soma katika Shule hiyo.
Naye Mwalimu
mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Elijali Waritu amesema kuwa shule hiyo imejipanga kuendelea
kutoa elimu bora na kufanya vizuri kitaaluma huku akiwaomba wazazi na walezi
kujenga utamaduni yakutembelea shule hiyo ili waweze kuona maendeleo ya watoto
wao.
Wahitimu wa darasa la awali SAPPS wakiwa kwenye picha ya pamoja . Wahitimu wa darasa la awali SAPPS wakionyesha burusani. Wahitimu wa darasa la awali SAPPS wakitoa burudani.Wahitimu wa darasa la awali SAPPS wakiwa kwenye mahafali.
0 Comments