6/recent/ticker-posts

MHE.KATAMBI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA UVCCM SHINYANGA MJINI ,ASAIDIA KUTATUA VIKWAZO VINAVYO WAKWAMISHA VIJANA KUPATA AJIRA

  Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu, Mhe.Patrobas Katambi akizungumza kwenye kikao cha baraza la UVCCM wilaya ya Shinyanga mjini.
Na Amo Blog Shinyanga 

Kikao cha Baraza la Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Shinyanga mjini Mkoani Shinyanga kimefanyika leo juma pili Desemba 17,2023 kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali ya kujenga umoja huo na Chama Cha Mapinduzi pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili vijana.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mgeni rasmi ambaye ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Mhe.Patrobas Katambi amewataka vijana kuacha kuchezea ujana wao kwa kujiingiza kwenye makundi yasiyofaa kama vile kukaa vijiweni lakini pia kuacha kutumia madawa ya kulevya hali inayo weza kuwarudisha nyuma kimaendeleo .
Katambi amesema mtaji namba moja wa kijana ni kuwa na afya njema,kwani ukijitunza na kuwa na afya njema utafanya kazi na kujipatia kipato, lakini afya yako ikiwa lege lege haina afya huwezi ukajumuika na watu huwezi ukafanya kazi,hivyo ni vizuri wajilinde.

"Niwaombe vijana wangu mjitambue muwe na subira mjitambue na kujua  kuwa nyinyi ni vijana mkijitambua hamuwezi kukimbilia kwenye madawa ya kulevya na bangi, hivyo niwaombe muwe na uzalendo, msimame vizuri kwenye elimu zenu au kwenye kazi zenu,"amesema Katambi.

" Tukilinde chama chetu kwa gharama yeyote tusikubali kurudi nyuma tufanye kazi kwa ushirikiano na mnatakiwa kuwa na ndoto na malengo, shabaha namakusudio na kuwana elimu dini,kwani Mungu ametupa talanta kila mmoja hivyo tuzitumie talanta zetu,"amesema Katambi

"Mmesema mna miradi 23 vikiwemo vyumba vya vibanda 23 vya kudumu na ukiwemo ujenzi wa nyumba ya katibu nitashirikiana nanyi kwa kutoa mchango wangu, sitawaangusha nitaendelea kufanya mimi kama mbunge nitatafuta fedha sehemu mbalimbali ili kuhakikisha tunashirikiana katika kuumaliza miradi hii na kuhakikisha inafanya kazi,"amesema Katambi.
Mhe.Katambi ameahidi kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana ikiwemo kukaa na wasimamizi wa miradi ya maendeleo na kuwapa maagizo ya kutoa kipaumbele  kwa kuajili vijana wazawa katika utekelezaji wa miradi hiyo

Naye Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Jonathan Madete amemshukuru Mhe.Katambi kwa kutenga mda wake na kushiriki katika kiikao cha kawaida cha baraza la vijana maana kufika kwake kutasaidia kujibu hoja ya changamoto zinazo wakabiri vijana hususani katika sekta ya ajira 

Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga mjini Jonathan Madete amewataka vijana kuendelea kukipambania Chama Cha Mapinduzi CCM ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Wanachama wanalipa ada kwa wakati, ikiwa ni pamoja na kushirikiana kwa pamoja kufanya kazi za chama pale wanapohitajika.

Aidha Madete amewataka vijana kukilinda Chama Cha Mapinduzi kwa Nguvu zao zote ili waweze kukivusha salama Chama  katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa ,na uchaguzi mkuu utakao fanyika mwaka 2025  katika kuhakikisha anachaguliwa kiongozi anaye jali na kusikiliza kero za wananchi.

Naye katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga mjini Naibu Katalambula akiwakilisha taarifa yake katika baraza hilo amewataka vijana kusimamia chama kwa nguvu zote ili kuhakikisha mwaka 2025 kinapata ushindi mkubwa wa kishindo, na kila kijana ahakikishe analipa ada na kuweza kuwaeleza wananchi kazi zinazosimamiwa na chama chama cha mapinduzi CCM.

Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu, Patrobas Katambi akizungumza kwenye kikao cha baraza la UVCCM wilaya wila ya Shinyanga mjini
Mwenyekiti wa Umoja wa vijana UVCCM Shinyanga mjini Jonathan Madete akizungumza kwenye kikao cha baraza
Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu, Patrobas Katambi akizungumza kwenye kikao cha baraza la UVCCM wilaya
Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu, Patrobas Katambi akizungumza kwenye kikao cha baraza la UVCCM wilaya

Mwenyekiti wa Umoja wa vijana UVCCM Shinyanga mjini Jonathan Madete akizungumza kwenye kikao cha baraza
Mwenyekiti wa Umoja wa vijana UVCCM Shinyanga mjini Jonathan Madete akizungumza na katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula
Wajumbe wa baraza la jumuiya ya Vijana UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa kwenye kikao
Wajumbe wa baraza la jumuiya ya Vijana UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa kwenye kikao
Wajumbe wa baraza la jumuiya ya Vijana UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa kwenye kikao
Wajumbe wa baraza la jumuiya ya Vijana UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa kwenye kikao
Mwenyekiti wa Umoja wa vijana UVCCM Shinyanga mjini Jonathan Madete akizungumza na Mhe.Patrobas Katambi mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini 
Katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Ally Majeshi akizungumza jambo mbele ya Mbunge wa jimbo hilo Patrobas Katambi

Mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya vijana CCM Piter Frank akizungumza kwenye baraza hilo

Post a Comment

0 Comments