6/recent/ticker-posts

NSSF WATOA MAFUNZ0 KWA WAJASIRIAMALI ,VIONGOZI NA WAFANYAKAZI ZAIDI YA 800 SHINYANGA

Mackdonald Maganga kutoka NSSF makao makuu akitoa elimu kwa wajasiliamali ,wafanyakazi na viongozi zaidi ya 800 Shinyaga juu ya umuhimu wa kujiunga na NSSF.

Na Amo Blog Shinyanga.

Uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii NSSF umeshiriki mkutano ulio andaliwa na mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mhe.Patrobas Katambi na kutoa elimu kwa baadhi ya Wajasiriamali,wafanyakazi na Viongozi mbalimbali juu ya umuhimu wakujiunga na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii NSSF .

Mkutano huo umefanyika leo decemba 21, 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga, ambapo ilitolewa elimu mbalimbali za kijasiriamali, usalama mahali pa kazi, walemavu, pamoja na dhana ya hifadhi ya jamii kwa kujiwekea mafao ya uzeeni.

Akitoa elimu hiyo Mackdonald Maganga kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii NSSF makao makuu amewaomba washiriki hao kutumia mafunzo waliyo yapata kubadili mtazamo na fikra zao kwa kuchukua maamuzi ya kujiunga na NSSF maana kwa sasa imeboresha huduma zake na kuwearuhusu wajasiliamali kujiwekea akiba kwa kutunza fedha kidogo kidogo ili fedha hizo ziweze kuwanufaisha baadae.

Nao baadhi ya washiriki wamkutano huo wameupongeza uongozi wa NSSF kwakutoa elimu hiyo maana watakuwa mabalozi wa kuwahamasisha watu wengine ili waweze kujiunga na mfuko huo na kujiwekea akiba itakayo wasaidia uzeeni.
Mackdonald Maganga kutoka NSSF makao makuu akitoa elimu kwa wajasiliamali ,wafanyakazi na viongozi zaidi ya 800 Shinyaga juu ya umuhimu wa kujiunga na NSSF.
Picha ya pamoja baada ya zoezi la utoaji wa elimu kumalizika.
Elimu ikiendelea kutolewa kwa wasdhiriki.

Elimu ikiendelea kutolewa kwa wasdhiriki.

Post a Comment

0 Comments