6/recent/ticker-posts

MWENYEKITI UVCCM SHINYANGA MJINI MADETE AFUNGUKA CHANGAMOTO ZINAZO WAKABILI VIJANA ,MHE.KATAMBI AWATAKA WASIMAMIZI WA SGR NA UWANJA WANDEGE KUWAPA KIPAUMBELE WANASHINYANGA

Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM Jonathan Madete akimkaribisha mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mhe.Patrobas Katambi  kwa ajili ya kuzungumza na UVCCM, 

Na Amo Blog Shinyanga 

Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga mjini Jonathan Madete amewataka vijana kuendelea kukipambania Chama Cha Mapinduzi CCM ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Wanachama wanalipa ada kwa wakati, ikiwa ni pamoja na kushirikiana kwa pamoja kufanya kazi za chama pale wanapohitajika.

Madete ametoa rai hiyo leo kwenye baraza la UVCCM wilaya ya Shinyanga mjini wakati wakikao cha kawaida cha baraza la vijana walicho keti kwa ajili ya kujadili mafanikio na changamoto zinazo wakabili katika baraza hilo ili ziweze kupatiwa ufumbuzi 

Madete amewataka vijana kukilinda Chama Cha Mapinduzi kwa Nguvu zao zote ili waweze kukivusha salama Chama  katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa ,na uchaguzi mkuu utakao fanyika mwaka 2025  katika kuhakikisha anachaguliwa kiongozi anaye jali na kusikiliza kero za wananchi.

Pia Madete amemuomba Mhe.Katambi kusaidia kutatua changamoto zinazo wakabili vijana ikiwemo changamoto ya baadhi ya wasimamizi wa miradi inayo tekelezwa Shinyanga kushindwa kuwapa fursa vijana katika utekelezaji wa miradi hiyo

Naye katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga mjini Naibu Katalambula akiwakilisha taarifa yake katika baraza hilo amewataka vijana kusimamia chama kwa nguvu zote ili kuhakikisha mwaka 2025 kinapata ushindi mkubwa wa kishindo, na kila kijana ahakikishe analipa ada na kuweza kuwaeleza wananchi kazi zinazosimamiwa na chama chama cha mapinduzi CCM.


"Kila kijana afanye wajibu wake maagizo haya tunayowapa mhakikishe mnayafanyia kazi, ili siku tutakayokutana mlete mrejesho wa kazi yenu, niwaombe sana myazingatie haya yote, pia simamieni chama cha mapinduzi huku mkifanya kazi kwa ushirikiano katika kukijenga chama chetu,"amesema Katalambula.

Kwa upande wake  mbunge wa jimbo la Shinyanga ambaye pia ni naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira vijana na wenye ulemavu, Patrobas Katambi ameitaka Jumuiya ya vijana Wilaya ya Shinyanga mjini kuacha kujiunga na vikundi visivyokuwa na maadili mema vinavyo tumia madawa ya kulevya badala yake wakemee tabia hizo na waweze kujitunza.

Katambi amesema mtaji namba moja wa kijana ni kuwa na afya njema,kwani ukijitunza na kuwa na afya njema utafanya kazi na kujipatia kipato, lakini afya yako ikiwa lege lege haina afya huwezi ukajumuika na watu huwezi ukafanya kazi,hivyo ni vizuri wajilinde.

"Niwaombe vijana wangu mjitambue muwe na subira mjitambue na kujua  kuwa nyinyi ni vijana mkijitambua hamuwezi kukimbilia kwenye madawa ya kulevya na bangi, hivyo niwaombe muwe na uzalendo, msimame vizuri kwenye elimu zenu au kwenye kazi zenu,"amesema Katambi.

" Tukilinde chama chetu kwa gharama yeyote tusikubali kurudi nyuma tufanye kazi kwa ushirikiano na mnatakiwa kuwa na ndoto na malengo, shabaha namakusudio na kuwana elimu dini,kwani Mungu ametupa talanta kila mmoja hivyo tuzitumie talanta zetu,"amesema Katambi

"Mmesema mna miradi 23 vikiwemo vyumba vya vibanda 23 vya kudumu na ukiwemo ujenzi wa nyumba ya katibu nitashirikiana nanyi kwa kutoa mchango wangu, sitawaangusha nitaendelea kufanya mimi kama mbunge nitatafuta fedha sehemu mbalimbali ili kuhakikisha tunashirikiana katika kuumaliza miradi hii na kuhakikisha inafanya kazi,"amesema Katambi.
Mhe.Katambi ameahidi kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana ikiwemo kukaa na wasimamizi wa miradi ya maendeleo na kuwapa maagizo ya kutoa kipaumbele  kwa kuajili vijana wazawa katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Mwenyekiti wa Umoja wa vijana UVCCM Shinyanga mjini Jonathan Madete akizungumza kwenye kikao cha baraza
Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu, Patrobas Katambi akizungumza kwenye kikao cha baraza la UVCCM wilaya
Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu, Patrobas Katambi akizungumza kwenye kikao cha baraza la UVCCM wilaya
Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu, Patrobas Katambi akizungumza kwenye kikao cha baraza la UVCCM wilaya
Mwenyekiti wa Umoja wa vijana UVCCM Shinyanga mjini Jonathan Madete akizungumza kwenye kikao cha baraza
Mwenyekiti wa Umoja wa vijana UVCCM Shinyanga mjini Jonathan Madete akizungumza na katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula
Wajumbe wa baraza la jumuiya ya Vijana UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa kwenye kikao
Wajumbe wa baraza la jumuiya ya Vijana UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa kwenye kikao
Wajumbe wa baraza la jumuiya ya Vijana UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa kwenye kikao
Wajumbe wa baraza la jumuiya ya Vijana UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa kwenye kikao
Mwenyekiti wa Umoja wa vijana UVCCM Shinyanga mjini Jonathan Madete akizungumza na Mhe.Patrobas Katambi mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini 
Katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Ally Majeshi akizungumza jambo mbele ya Mbunge wa jimbo hilo Patrobas Katambi

Mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya vijana CCM Piter Frank akizungumza kwenye baraza hilo

Post a Comment

0 Comments