6/recent/ticker-posts

WAZIRI BASHUNGWA ABISHA HODI SHINYANGA AITAKA TANROADS KUFANYA MATENGENEZO YA BARABARA ZA CHANGARAGWE

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akiendelea na ukaguzi wa Barabara.

Na Mwandishi Wetu Amo Blog Shinyanga 

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameuagiza uongozi wa  Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS)  kuhakikisha barabara za changarawe zinapewa kipaumbele kama ilivyo kwenye barabrara za lami, kwa kuzifanyia matengenezo ya mara kwa mara ili zipitike kipindi chote cha mwaka. 

Ametoa agizo hilo leo tarehe 08 Disemba 2023 wakati akikagua Barabara ya  Old Shinyanga - Solwa pamoja na Barabara ya Solwa - Kahama na miundombinu mingine katika Mkoa wa Shinyanga ambayo imeharibika na mvua zinazoendelea kunyesha. 

Akiwa katika ukaguzi huo, ameagiza barabara ya  kutoka Old Shinyanga  - Shilabela eneo korofi  la Selamagazi ambako ni makao makuu ya Halmashauri ya Shinyanga Vijjini (km 33) iwe kwenye vipaumbele mahsusi ya  kuwekwa lami kwa mwaka ujao wa fedha, ili iweze kuhudumia Halmashauri pamoja na Hospitali ya Wilaya.

 Kuhusu kipande cha barabara kilichopo eneo la Center ya Solwa (mita 600) ambacho ujenzi wake umesimama, Waziri Bashungwa amemuagiza Mkurugenzi wa Matengenezo Tanroads, Dk. Christina Kayoza kuhakikisha ujenzi wake unaanza haraka. 

"Mkurugenzi wa matengenezo ninyi ndio mnafanya kazi kunisaidia siwezi kwenda kila kona ya nchi, maeneo ambapo tunatengeneza mita 600,  mita 500, kilometa moja, mpaka nifike niongee na wananchi ndio mchukue hatua, sasa kajipange na idara yako ya matengenezo kwa kushirikiana na Meneja wa Tanroads Mkoa wa Shinyanga, kesi kama niliyoikuta hapa Solwa sitaki kusikia sehemu yoyote," alisema Waziri Bashungwa. 

Katika hatua nyingine, Waziri Bashungwa amewataka wanafunzi wahitimu wa uhandisi waliopo kwenye  programu ya mafunzo ya SEAP kuwekwa kwa mfumo wa kuwapata ambao utakuwa wa wazi na fursa kwa wote bila upendeleo.

 Pia, Ameitaka Wizara ya Ujenzi kusimamia, kuja na mkakati wa kuongeza wigo wa kupata vijana zaidi wahitimu wa fani husika kwa ajili ya mipango ya baadaye.

 Bashungwa amesema kwa miaka mitano ijayo kunauwezekano wa kutokea kwa uhaba wa Wahandisi wazoefu kwenye miradi ya ujenzi wa barabara na madaraja.

 Naye, Mkurugenzi wa Matengenezo kutoka TANROADS, Mhandisi Christina Kayoza, amemhakikishia Waziri Bashungwa kwambandani ya muda mfupi watakamilisha ukarabati wa kipande hicho cha barabara kilichopo eneo la Center ya Solwa (mita 600). 

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akiendelea na ukaguzi wa Barabara Shinyanga .
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akiendelea na ukaguzi wa Barabara Shinyanga .

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akiendelea na ukaguzi wa Barabara Shinyanga .
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akizungumza na wananchi wakati wa ukaguzi wa Barabara Shinyanga .
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akizungumza na wananchi wakati wa ukaguzi wa Barabara Shinyanga .
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akizungumza na wananchi wakati wa ukaguzi wa Barabara Shinyanga .


Post a Comment

0 Comments