6/recent/ticker-posts

MAHAKAMA KUU KANDA YA SHINYANGA YAENDELEA KUPUNGUZA MLUNDIKANO WA MASHAURI ,JAJI MAHIMBALI AELEZA WALIVYO JIPANGA MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA JANUARI 24


 Mahakama kuu kanda ya Shinyanga, imesema mashauri ya makosa ya jinai yanayohusisha mauaji pamoja na migogoro ya ardhi ni kati ya mashauri mengi yanayoongoza kufunguliwa katika Mahakama mbalimbali za kanda kwa kipindi cha Mwaka uliopita wa 2023.

Na Mapuli Kitina Misalaba

 Taarifa hiyo imetolewa na Jaji mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Shinyanga Frank Habibu Mahimbali, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kuelekea maadhimisho ya wiki ya sheria nchini, ambayo kwa Kanda ya Shinyanga yatafanyika katika uwanja wa Zimamoto Nguzonane mjini Shinyanga.

 Jaji Mahimbali amebainisha kuwa, mashauri mengi ya migogoro ya ardhi yanachangiwa na uelewa mdogo wa wananchi kuhusu sheria ya matumizi na umiliki wa ardhi ambapo yale ya mauaji yanatokana hasa na imani za kishirikina.

 Kwa mahakama kuu kanda ya Shinyanga mashauri mengi yanayofunguliwa hapa ni makosa ya jinai na mashauri ya mauaji hayo ni mashauri mengi sana ambayo yanafunguliwa ambayo yanahusisha mauaji mbalimbali ya watu yakiwemo ya tuhuma za ushirikina na kuthurumiana mali lakini ya kishirikina ndiyo mengi sana lakini mashauri mengine ambayo yanafuatia niya migogoro ya ardhi hayo ni mengi sana ukilinganisha na mashauri mengine ambapo kitakwimu hayo ndiyo yanaongoza yanafuatia mashauri ya mauaji kwanini mashauri ya migogoro ya ardhi yako mengi mojawapo ya sababu ni elimu ndogo kwa wananchi kuhusiana na sheria zinazosimamia umiliki na utatuzi wa migogoro ya ardhi”. Amesema Jaji Mahimbali

 Akizungumzia maadhimisho ya wiki ya sheria ambayo yanafanyika kuanzia Januari 24 hadi 30 Mwaka huu, Jaji Mahimbali amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa zimamoto, ili kupata elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria, ikiwemo sheria za ardhi, Mirathi, Ndoa, makosa ya jinai, ushughulikiaji wa malalamiko pamoja na ufunguaji wa kesi kwa njia ya mtandao.

 Mahakama kuu kanda ya Shinyanga itashirikiana na wadau mbalimbali katika kutoa elimu kwenye Maadhimisho hayo, ikiwemo ofisi ya Taifa ya Mashtaka, wakili mkuu wa serikali, mawakili wa kujitegemea, kituo cha msaada wa kisheria, Jeshi la polisi, jeshi la Magereza, NIDA, RITA, TRA,pamoja na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU.

 Wadau wengine watakaoshiriki ni madalali wa Mahakama, mawakili wa kujitegemea, mabaraza ya ardhi na Nyumba, ofisi ya kamishna wa ardhi na utatuzi wa migogoro ya ardhi, utatuzi wa migogoro ya kazi na ajira kazini kutoka CMA, huduma za upimaji wa magonjwa yasiyoambukizwa kama vile Presha, Kisukari, zitolewazo na wataalam kutoka Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. 

    Mhe.Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya shinyanga Frank Habibu Mahimbali.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Shinyanga, Mhe. Warsha Ng’humbu.

Mtendaji wa Mahakama kuu kanda ya Shinyanga  Bi. Mavis Miti

 


 



Post a Comment

0 Comments