6/recent/ticker-posts

REDCROSS SHINYANGA YA WAPIGA MSASA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII NA VOLUNTEER

Viongozi wa Tanzania Red Cross Society mkoa wa Shinyanga Wakishirikiana na Ofisi ya Mganga mkuu kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii na Volunteer juu ya magonjwa ya mlipuko.
Na Amo Blog Shinyanga .

Katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko Uongozi wa Tanzania Red Cross Society mkoa wa Shinyanga Wakishirikiana na Ofisi ya Mganga mkuu wametoa mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii na Volunteer ili kuwajengea uwezo wa kwenda kutoa elimu katika jamii juu ya magonjwa ya mlipuko.

Mafunzo hayo yamefanyika March 18,2024 katika ukumbi wa Karena Hotel na kushirikisha washiriki 50 kutoka wilaya ya Shinyanga,Kishapu na Kahama,mafunzo ambayo yatadumu kwa muda siku tatu.

Akieleza lengo la kutoa mafunzo hayo mratibu wa Redcross mkoa wa Shinyanga Adelina Apolinary amesema kuwa wameamua kushirikiana na ofisi ya mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga kuwajengea uwezo wahudumu wa afya ngazi ya jamii pamoja na Volunteer juu ya namna ya kupambana na magonjwa ya mlipuko ili waende kutoa elimu katika jamii juu ya namna ya kujikinga na magonjwa hayo.

Adelina amesema kuwa mafunzo hayo yameshirikisha washiriki kutoka Wilaya ya Kahama,Shinyanga,na Kishapu ambapo baada ya mafunzo hayo washiriki watakwenda kutoa mafunzo katika maeneo yao.

Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga(Faustine Mlyutu) amewapongeza Redcross kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika mapambano ya magonjwa ya mlipuko.Ambapo amewataka washiriki kushiriki kikamilifu katika mafunzo hayo ili waweze kupata maarifa na ujuzi utakaowasaidia kwenda kuisaidia jamii katika maeneo yao.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Mary Charles,Venance Mahona na Pendo Maguzu wamekipongeza chama cha msalaba mwekundu na ofisi ya Mganga Mkuu kwa kutoa mafunzo hayo ambayo yatawasaidia kwenda kutoa elimu katika jamii na kuachana na utamaduni wakutoa elimu kwa kutumia uzoefu huku wakiahidi kwenda kuwa mabalozi katika jamii zao.

Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Fuustine Mlyutu akitoa elimu kwa washiriki wa mafunzo.

Mratibu wa Redcross Mkoa wa Shinyanga Adelina Apolinary akiendelea na zoezi la kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii na Volunteer.
Mratibu wa afya kwa umma mkoa wa Shinyanga Mwita Richard akitoa elimu kwa washiriki wa mafunzo.
Wahudumu wa afya ngazi ya jamii na Volunteer wakiendelea kupata mafunzo katika ukumbi wa Karena hotel yanayo tolewa na Viongozi wa Redcroos Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Ofisi ya mganga mkuu.

 Mkufunzi kutoka Redcross Juliana Benard akiendelea na zoezi la kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii na Volunteer.
Viongozi wa Tanzania Red Cross Society mkoa wa Shinyanga Wakishirikiana na Ofisi ya Mganga mkuu kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii na Volunteer juu ya magonjwa ya mlipuko.
Mratibu wa afya kwa umma mkoa wa Shinyanga Mwita Richard akitoa elimu kwa washiriki wa mafunzo.

Post a Comment

0 Comments