6/recent/ticker-posts

MCHUNGAJI KANUNU KUTOKA KANISA LA NGUVU YA NENO BAPTIST NYANENDE MANISPAA YA SHINYANGA ,AWATAKA WAUMINI WA KANISA HILO KUTOKATA TAMAA


Mchungaji wa kanisa la Nguvu ya neno Baptist Nyanende Manispaa ya Shinyanga ambaye pia ni mwangalizi wa makanisa ya Nguvu ya neno Mchungaji Renatus Kanunu ewaka amewaka Wakristo kutokata tamaa wanapokabiliwa na changamoto katika maisha yao, waamini Mungu yupo kwa ajili yao.

Mchungaji Kanunu amesema hayo Marchi 31,2024 kwenye maadhimisho ya siku ya Pasaka wakati akihitimisha kongamano lililo Shirikisha waumini kutoka mikoa ya Shinyanga ,Simiyu na Tabora kwa lengo la kusifu na kupata mafundisho ya neno la mungu.

Aidha Mchungaji Kanunu amesema kuwa kila mkristo anaye mtegemea mwenyezi mungu ataendelea kuinuliwa katika viwango vya juu kwa kuwa yesu kristu amefufuka kwa ajili ya kuwakomboa wanadamu hivyo nivyema kila mkristo akaendelea kumtegemea mwenyezi mungu kuliko kumtegemea mwanadamu.

Kwa upande wao baadhi baadhi ya waumini walio shiriki kongamano hilo wamesema kuwa wamejifunza mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kubadilisha misha yao iwapo watamtegemea mwenyezi mungu na kukumbuka kuwa yesu kristo amefufuka kwa ajili ya kuwakomboa wanadamu wenye changamoto na shida mbalimbali huku wakiomba kongamano hilo liendelee kufanyika kila mwaka.
Mchungaji Renatus Kanunu Mwangalizi wa Makanisa ya Nguvu ya neno Baptist akiongoza ibaada ya pasaka..Waumini wa kanisa la Nguvu ya neno Baptist Nyanende Shinyanga wakiwa kwenye ibaada ya Pasaka.
Waumini wa kanisa la Nguvu ya neno Baptist Nyanende Shinyanga wakiwa kwenye ibaada ya Pasaka.Waumini wa kanisa la Nguvu ya neno Baptist Nyanende Shinyanga wakiwa kwenye ibaada ya Pasaka.Waumini wa kanisa la Nguvu ya neno Baptist Nyanende Shinyanga wakiwa kwenye ibaada ya Pasaka.Waumini wa kanisa la Nguvu ya neno Baptist Nyanende Shinyanga wakiwa kwenye ibaada ya Pasaka.

Post a Comment

0 Comments