6/recent/ticker-posts

DC WAKILI MTATIRO ABISHA HODI KATA YA USANDA ,ASIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI WAKATA HIYO

Wakili Julius Mtatiro akisikiliza na kutatua kero za wananchi wa kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Na Amojmedia Blog Shinyanga.

Watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani humo wametakiwa kujenga utamaduni wakusikiliza kero za wananchi na kuzitatua kwa wakati.

Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa lengo la kusikiliza kero zinazo wakabili wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

Wakili Mtatiro amesema kuwa Rais Samia Suluhu 
Hassan anataka wananchi wahudumiwe, wasikilizwe kero zao kwa kutendewa haki, kwani mtumishi ukimtendea haki mwananchi na wewe unapata haki kwa Mungu, hivyo ni vyema wananchi wakasaidiwa kwa kutatuliwa kero zao.

"Wananchi wetu wakitendewa haki inakuwa haki hadi kwa mungu na mimi kwenye suala la haki sina mswalia mtume , nimetumwa hapa kwa ajili ya kufanya kazi na kusimamia haki za wananchi maana 
kazi hii niliyopewa ni dhamana ya muda mfupi tu, ambayo ni ya kumsaidia Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan  kutatua kero zao,,,"amesema Wakili Mtatiro.  

Aidha Wakili Mtatiro amewaomba wananchi wanao kabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji katika kata hiyo kuendelea kuwa wavumilivu wakati jitihada zakufikisha mtandao wamaji ya ziwa victoria katika kata ya Usanda zinaendelea kwa kuwa Rais Samia_Suluhu_Hassan yuko kazini.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi ambao kero zao zimepatiwa ufumbuzi wamempongeza Wakili Mtatiro kwa kuendelea kuwafata wananchi kwenye maeneo yao na kusikiliza kero zanazo wakabili na kuzitaftia ufumbuzi huku wakiahidi kuendelea kutoa ushirikiano .
Wakili Julius Mtatiro akisikiliza na kutatua kero za wananchi wa kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Wananchi wa kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakijiandaa kutoa kero zao kwa Wakili Mtatiro.
Wananchi wa kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakijiandaa kutoa kero zao kwa Wakili Mtatiro.

Post a Comment

0 Comments