6/recent/ticker-posts

NTOBI ASHINDA TENA UENYEKITI CHADEMA SHINYANGA

  

Emmanuel Ntobi, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Shinyanga baada ya ushindi.

Chanzo Malunde 1 Blog

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Shinyanga , Emmanuel Ntobi, ameshinda kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho mkoani humo, katika uchaguzi wa Machi 28, 2024. 

Katika uchaguzi huo Ntobi alikuwa akichuana na Peter Machaga ambaye alipata kura 26, Ntobi 26 na Thadei Mwati Kura 8. Na ikalazimu kurudiwa kwa duru ya pili ambapo Ntobi alichuana na Machaga na kuibuka na kura 33 sawa na asilimia 55, na Machaga kuibuka na kura 27.

Hivyo Msimamizi mkuu wa uchaguzi Suzani Kiwanga (ambaye ni mjumbe wa kamati kuu CHADEMA) alimtangaza Ntobi kuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga.

Ntobi anakuwa ni Mwenyekiti wa Chama hicho kwa kipindi cha pili 2024 hadi 2029.

Post a Comment

0 Comments