6/recent/ticker-posts

TAMASHA LA NMB KIJIJI DAY LAFANA SHINYANGA ,MAMIA WAJITOKEZA KUFUNGUA AKAUNTI

Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Manonga Gadiel Sawe akizungumza na wananchi walio jitokeza katika Tamasha la NMB Kijiji Day.

            Na Amojmedia Blog

Benki ya NMB Tawi la Manonga kwa kushiorikiana na Uongozi wa Benki hiyo Kanda ya Magharibi imeendesha Tamasha la NMB Kijiji Day Katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mkoani humo kwa lengo la kuhamasisha Watanzania kuhifadhi fedha katika Taasisi za fedha pamoja na kukata Bima ili kulinda shughuli zao ikiwemo biashara pindi wanapopatwa na majanga mbalimbali yakiwemo ya moto, mafuriko na ajali zinazoweza kusababisha madhara na kusababisha kuyumba kiuchumi.

Tamasha hilo lililo kwenda sanjari na utoaji elimu na ushauri kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kuwa na huduma ya NMB Pesa akaunti pamoja na Bima umefanyika leo Jumatatu Aprili 22,2024 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Didia Halmashauri ya Walaya ya Shinyanga na kuwakusanya Mamia ya watanzania walio jitokeza kwa ajili ya kupata huduma zinazo tolewa na Benki ya NMB.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Manonga Gadiel Sawe amesema kuwa lengo la tamasha la NMB Kijiji Day ni kutoa elimu ya masuala ya Akaunti pamoja na bima, kutoa ushauri pamoja na kuuza bima mbalimbali ikiwemo Bima ya Faraja inayolenga zaidi kutoa mafao ya pole kwa mwananchi anapopatwa na changamoto ya msiba au ulemavu ambapo mteja anajiunga kwa Shilingi 200/= na anapata fao kuanzia Sh.milioni 1 hadi 6.

“Ndugu zangu hivi karibuni mmekuwa mkishuhudia majanga ya moto, mafuriko na ajali mbalimbali, hivyo ni vyema ukawa na bima ili unapopatwa na majanga usipate hasara na kuepuka kuyumba kiuchumi. Njoo ukate bima kwa ajili yako na mali zako. NMB inashirikiana na kampuni mbalimbali za utoaji bima”,amesema Sawe.


Nao baadhi ya wananchi pamoja na wanamichezo  waliofanikiwa kufikiwa na Benki ya NMB na kuwapatia elimu ya umuhimu wa kuwa na akaunti pamoja na Bima wameishukuru Benki ya NMB kwa kupatia elimu ya umuhimu wa kuwa na akaunti za benki hiyo pamoja na bima na kuahidi kukata bima ili wao na mali zao ziwe salama na kwamba watahamasisha pia wananchi wengine wakate bima.

Hata hivyo tamasha hilo lilishilikisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wamiguu ,kukimbiza baiskeli,kukimbiza kuku pamoja na kucheza Lede ambapo washindi wote waliondoka na zawadi kutoka Benki ya NMB.















































 

Post a Comment

0 Comments