6/recent/ticker-posts

DC WAKILI MTATIRO ATOA SIKU 7 BARABARA YA HOSPITALI YA RUFAA MWAWAZA IFANYIWE MATENGENEZO YA HARAKA,WANANCHI WAJITOKEZA KUELEZA KERO ZAO

DC MTATIRO AMESIKILIZA KERO ZA WANANCHI NA KUTOA MAAGIZO BARABARA YA HOSPITALI YA RUFAA MWAWAZA IFANYIWE MATENGENEZO YA HARAKA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKUU wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro, ameendelea na ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na kutoa maagizo kwa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) wilaya ya Shinyanga, kwamba hadi kufika Aprili 10 mwaka huu Barabara ya kutoka Ndala kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa iliyopo Mwawaza iwe imeshafanyiwe Matengenezo ya haraka.

Amebainisha hayo leo Aprili 3,2024 kwenye Mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za Wananchi wa Manispaa ya Shinyanga, uliofanyika katika Soko Kuu la Manispaa hiyo.

Amesema kila anapofanya Mikutano ya hadhara kusikiliza kero za Wananchi. kilio chao kikubwa ni ubovu wa barabara hiyo ya kutoka Ndala kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwawaza, kero ambayo ni muhimu sababu inagusa maisha ya watu kutokana na umuhimu wa barabara hiyo.

“Naiagiza TARURA hadi kufikia Terehe 10 Mwezi huu, Barabara hiyo ya kutoka Ndala kwenda Hospitali ya Rufaa Mwawaza iwe imeshafanyiwa Matengezo ya haraka kupitia fedha za dharura, Barabara hii ni muhimu sana sababu inagusa maisha ya watu kutokana kufuata huduma za Matibabu katika Hospitali ya Rufaa,”amesema Mtatiro.

“Kero zingine zipo kwenye uwezo wetu kuzitatua siyo mpaka aje Waziri Mkuu ndipo itatuliwe kwa hili TATURA tutagombana, na Mkishindwa kuifanyia Matengenezo na Mpigia Simu Mkurugenzi Mkuu wa TARURA au Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa, hatuwezi kuwa na Barabara Mbovu inayokwenda Hospitali,”ameongeza.

Aidha,akijibu Kero ya Mwananchi Hussein Pembe kuhusu kupewa Kiwanja na Manispaa chenye Migogoro baada ya kuhamishwa kwenye eneo la Barabara, ameagiza kwamba Mwananchi huyo apewe Kiwanja kingine na ndani ya Mwezi Mmoja apewe Majibu.

Amesema kero zingine atazifanyia kazi kwa kutuma Timu ya Wataalamu wake ambayo ameiunda, ikiwamo kushughulikia Migogoro ya Ardhi ya Mipaka, Maeneo ya Wazi ambayo yameuzwa na kujengwa nyumba, huku akiagiza Halmashauri kukamilisha Ujenzi wa Soko Kuu la Manispaa ya Shinyanga na ujenzi wa “Parking” ya Malori.

“Wananchi msiwe na wasiwasi kero zenu zote zitashughulikiwa uzuri Shinyanga tunatimu nzuri ya viongozi, na Mkurugenzi wenu wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze namfahamu ni mchapakazi sana tunafahamiana tangu tukiwa Chuo Kikuu Dar Es Salaamu, pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,”amesema Mtatiro.

Nao baadhi ya Wananchi waliwasilisha kero zao kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga zikiwamo za Migogoro ya Ardhi, kugombea Mipaka, Malipo ya Fidia, kukosekana Maeneo ya “Packing” za Malori, Maeneo ya Wazi kuuzwa, na Ubovu wa Miundombinu ya Barabara ya kutoka Ndala kwenda Hospitali ya Rufaa Mwawaza.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akichukua kumbukumbu za kero ambazo zinawasilishwa na wananchi.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze akichukua kumbumbuku za kero ambazo zinawasilishwa na wananchi kwa ajili ya kuzijibu.

Viongozi mbalimbali na Wakuu wa Idara ya Halmashauri wakichukua kumbukumbu ya kero ambazo zinawasilishwa na wananchi kwa ajili ya kuja kuzijibu.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza na wananchi kwenye Mkutano wa hadhara na kujibu kero zao.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akiendelea kuzungumza na wananchi kwenye Mkutano wa hadhara na kujibu kero zao.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akiendelea kuzungumza na wananchi kwenye Mkutano wa hadhara na kujibu kero zao.

Wananchi wakiwasilisha kero zao kwenye Mkutano huo.

Wananchi wakiendelea kuwasilisha kero zao.

Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara wa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro wa kusikiliza kero zao na kupatiwa ufumbuzi.

Mkutano wa kusikiliza kero za wananchi ukiendelea.

Post a Comment

0 Comments