6/recent/ticker-posts

BENKI YA NMB TAWI LA MANONGA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI SHINYANGA

Afisa Masoko wa Benki ya NMB Tawi la Manonga Albin Mpona ameshiriki Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyo fanyika Mkoa wa Shinyanga na kuongozwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha ambapo maadhimisho hayo yamefanyika leo Mei 15,2024 na Kitaifa Maadhimisho hayo yalifanyika Mei 3 mwaka huu Jijini Dodoma na Mgeni Rasmi alikuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Aidha Mpona ametumia maadhimisho hayo kutoa elimu kwa waandishi wa habari na wadau wa habari walio shiriki katika maadhimisho hayo juu ya umuhimu wawadau na wanahabari kujiunga na huduma za benki ya NMB ikiwemo NMB Pesa Akaunti,Chap Chap Akaunti,Bima ya Faraja pamoja na kuwasii kuendelea kuteleza kidijitali wakiwa na Akaunti ya NMB 

Mpona  ameeleza kuwa NMB Pesa Akaunt ni Akaunti ya kidijitali na ya haraka zaidi ambayo ukiwa na kitambulisho chako na shilingi elfu moja (1000) unafungua akaunti , huku akisisitiza kuwa ukiwa na Akaunti ya NMB Unaweza ukapata manufaa ya fuatayo.

Hatahivyo Mpona ameeleza na mna Benki ya NMB inavyo shirikiana na wadau kutunza mazingira ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya nchi.

✅Mikopo isiyo na dhamana

✅Kutoa, kuweka au kutuma pesa

✅Kulipia bili

✅Kubwa zaidi; hakuna ada za kila mwezi

Yote kupitia simu yako tu (kitochi au simu janja).


 

Post a Comment

0 Comments