6/recent/ticker-posts

CDC NA AMREF TANZANIA ZASHIRIKIANA KUIMARISHA KINGA YA MAGONJWA YA MLIPUKO KATIKA WILAYA YA HANANG - MANYARA

 

Mgeni rasmi, Dkt. Mohamed Kodi ambaye ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Mkoani Manyara (wa kwanza kushoto) akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Hanang wakati wa uzinduzi rasmi wa maeneo maalum ya kunawia mikono yaliyojengwa na Shirika la Amref Tanzania, kupitia ufadhili wa Kituo cha serikali ya Marekani CDC Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Afya & TAMISEMI. Mkurugenzi wa Kitengo cha Ulinzi wa Afya, katika Kituo cha serikali ya Marekani cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) Tanzania, Dkt. Wangeci Gatei (wa 4 kulia) na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amref Tanzania, Dkt. Florence Temu (wa 3 kulia).


Maeneo hayo maalum kwa ajili ya kunawia mikono yamejengwa katika shule 4️ (3 za msingi na 1 sekondari) wilayani humo ikiwa ni sehemu ya kukinga jamii inayozunguka maeneo hayo na magonjwa ya mlipuko kufuatia janga la maporomoko ya udongo na mafuriko yaliyoikumba wilaya hiyo, Disemba 2023.
Mgeni rasmi Dkt. Mohamed Kodi (wa 6 kulia) na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ulinzi wa Afya, katika Kituo cha serikali ya Marekani cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) Tanzania, Dkt. Wangeci Gatei (wa 6 kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amref Tanzania, Dkt. Florence Temu (Wa 5 kulia) Pamoja na viongozi mbalimbali na wanajamii mara baada uzinduzi rasmi na makabidhiano ya maeneo hayo ya kunawia mkono, katika shule ya Msingi Ganana, Hananga DC, Manyara 03-5-2024.
Wanafunzi wa shule mbalimbali, wakiwa katika maeneo ya kunawia mikono, maeneo hayo yamejengwa katika shule 4️ (3 za msingi na 1 sekondari) wilayani humo ikiwa ni sehemu ya kukinga jamii inayozunguka maeneo hayo na magonjwa ya mlipuko kufuatia janga la maporomoko ya udongo na mafuriko yaliyoikumba Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara, Disemba 2023.
Picha ya pamoja na Mgeni rasmi, Dkt. Mohamed Kodi (wa 3 kulia) na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amref Tanzania, Dkt. Florence Temu (Wa 2 kulia), Mkurugenzi wa Kitengo cha Ulinzi wa Afya, CDC Tanzania, Dkt. Wangeci Gatei (wa 3 kushoto) Pamoja na viongozi mbalimbali na wanajamii mara baada uzinduzi rasmi na makabidhiano ya maeneo ya kunawia mkono, katika shule ya Msingi Ganana, Hananga, Manyara 03-5-2024.

**

Katika azma ya kuimarisha mbinu za kuzuia magonjwa ya mlipuko katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara nchini Tanzania baada ya maafa ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea Desemba 2023, Shirika la Amref Health Africa Tanzania, kwa msaada wa Kituo cha serikali ya Marekani cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) Tanzania) lakabidhi maeneo manne ya kunawia mikono katika shule za Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara. Maeneo hayo yaliojengwa kwa gharama ya dollar za kimarekani 15,592 yanalenga kuimarisha mbinu za kuzuia maambukizi ya magonjwa mbalimbali ya mlipuko katika maeneo ya umma, kwa kuzingatia miongozo ya Wizara ya Afya.

Katika hafla hiyo ya makabidhiano yalioyafanyika katika Shule ya Sekondari Ganana wilayani Hanang mkoani Manyara, Mkurugenzi Mkazi wa Amref Tanzania, Dkt.Florence Temu alisisitiza umuhimu wa mbinu jumuishi za kuimarisha magonjwa ya mlipuko katika jamii kupitia ufuatiliaji wa huduma za Maji na usafi wa mazingira (Water Sanitation and Hygiene - WASH) pamoja na Ufuatiliajiwa matukio na magonjwa ya mlipuko (Event-based Surveillance – EBS) na wilayani humo. Aliangazia maendeleo makubwa yaliyopatikana katika ufuatiliaji wa mapema na kukabiliana na vitisho vya afya ya umma katika kanda hiyo hasa magonjwa ya mlipuko, Kupitia msaada wa Kituo cha serikali ya Marekani (CDC) Tanzania.

Dk. Temu pia alitoa shukrani kwa ushirikiano kati ya Amref Tanzania na Kituo cha serikali ya Marekani (CDC) Tanzania, ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika kutoa ushauri na uhamasishaji katika uboreshaji wa huduma za Maji na usafiwa mazingira (Water Sanitation and Hygiene - WASH) pamoja na Ufuatiliajiwa matukio na magonjwa ya mlipuko (Event-based Surveillance - EBS) na hivyo kusababisha kuzuia magonjwa ya kuambukiza katika kanda.


Kwa upande wake Mgeni rasmi, Dkt. Mohamed Kodi ambaye ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Mkoani Manyara (wa kwanza kushoto) akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Hanang wakati wa uzinduzi rasmi wa maeneo maalum ya kunawia mikono, ameipongeza Serikali ya Tanzania, Kituo cha serikali ya Marekani cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) Tanzania na Amref Tanzania kwa juhudi zao za kuiunga mkono serikali katika kuimarisha Mfumo wa Ufuatiliaji wa Mazingira na Kuboresha Sekta ya Afya kupitia miradi mbalimbali ya afya nchini. Alisisitiza uwajibikaji wa utunzaji wa maeneo hayo na kusisitiza haja ya kuchukuliwa hatua za kisheria kwa yeyote atakayesababisha uharibifu au uzembe.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Ulinzi wa Afya, katika Kituo cha serikali ya Marekani cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) Tanzania, Dkt. Wangeci Gatei alisisitiza dhamira ya CDC Tanzania katika kuimarisha mbinu za kuzuia maambukizi ya magonjwa ya mlipuko nchini Tanzania kupitia juhudi za ushirikiano na serikali na washirika wa ndani. Alisisitiza lengo la kuisaidia Serikali ya Tanzania katika kuzingatia Kanuni za Kimataifa za Afya (2005) kupitia malengo ya Global Health Security Agenda (GHSA) 2024.


Hafla ya makabidhiano hayo ilihudhuriwa na wawakilishi kutoka Wizara ya Afya, Kituo cha serikali ya Marekani CDC Tanzania, Amref Tanzania, pamoja na viongozi wa serikali za mitaa, wahudumu wa afya ya jamii, walimu na wanafunzi. Ushirikiano kati ya Amref Tanzania na Kituo cha serikali ya Marekani CDC Tanzania unalenga kuimarisha mbinu za kuzuia maambukizi katika maeneo ya umma na kuchangia katika uboreshaji wa jumla wa afya ya umma katika eneo hilo.

Kufuatia maporomoko ya matope yaliyotokea mkoani Manyara, ambayo yamesababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao na kusababisha vifo vya watu wengi, Shirika la Amref Tanzania, kwa msaada kutoka Kituo cha serikali ya Marekani CDC Tanzania, linaendelea kushirikiana katika masuala ya uboreshaji wa huduma za Maji na usafi wa mazingira (Water Sanitation and Hygiene- WASH) pamoja na Ufuatiliaji wa matukio na magonjwa ya mlipuko (Event-based Surveillance - EBS) ili kuzuia magonjwa ya kuambukiza katika Wilaya ya Hanang. Katika viwango mbalimbali na kutoa usaidizi kwa onyo la mapema na kukabiliana na vitisho vya afya ya umma katika eneo hilo.

Post a Comment

0 Comments