Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mihayo Tabora Bw.George Fundi akikabidhi vifaa vya michezo kwa uongozi wa Elimu mkoa wa Tabora kwa niaba ya Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio.
Na Amojmedia Shinyanga
Benki ya NMB Kanda ya Magharibi imetoa msaada wa vifaa vya michezo pamoja na fedha kiasi cha shilingi milioni mbili Kwa uongozi wa Elimu mkoa wa Tabora kwa ajili ya wanafunzi watakao shiriki mashindano ya UMISETA ngazi ya kitaifa mkoani Tabora.
Msaada huo umekabidhiwa na Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mihayo Tabora Bw.George Fundi kwa niaba ya Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio.
Vifaa hivyo ni jezi za mpira wa Miguu ,Mpira wa mikono, mpira wa kikapu pamoja na michezo mingine huku wakikabidhi kiasi cha Shilingi milioni 2 kwa ajili ya kuwawezesha vijana walio chaguliwa kushiriki mashindano ya UMISETA Mkoani humo ili waweze kufanya vizuri katika mashindano hayo ,Pia ikiwa nisehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya michezo nchini.
Mashindano ya Umiseta yanatarajiwa kuzinduliwa kesho kitaifa katika uwanja wa Shule ya Sekondari Tabora Boys uliopo mkoani Tabora.
TAZAMA PICHA ZA MAKABIDHIANO HAPA CHINI.
0 Comments