6/recent/ticker-posts

JE? UMEBIMA !!!! NMB KANDA YA MAGHARIBI YAENDELEA KUWAKUMBUSHA WANANCHI KUKATA BIMA YA SH.200

Watanzania wametakiwa kuendelea kujiunga na huduma ya Bima inayo tolewa na Benki ya NMB ili kulinda shughuli zao ikiwemo biashara pindi wanapopatwa na majanga mbalimbali yakiwemo ya moto, mafuriko na ajali zinazoweza kusababisha madhara na kusababisha kuyumba kiuchumi.

Hayo yameelezwa na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio wakati akizungumza na Amojmedia juu ya umuhimu wawananchi kujiunga na huduma ya Bima ikiwa ni siku chache baada ya kuzindua Kampeni ya Umebima hafla iliyo fanyika katika Kituo cha Mabasi cha CDT Mjini Kahama Mkoani Shinyanga .

Aidha Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio ameeleza kuwa Kampeni ya Umebima bado inaendelea maana lengo la Kampeni hiyo ni kutoa elimu ya masuala ya bima, kutoa ushauri pamoja na kuuza bima mbalimbali ikiwemo Bima ya Faraja inayolenga zaidi kutoa mafao ya pole kwa mwananchi anapopatwa na changamoto ya msiba au ulemavu ambapo mteja anajiunga kwa Shilingi 200/= na anapata fao kuanzia Sh.milioni 1 hadi 6.


“Ndugu zangu hivi karibuni mmekuwa mkishuhudia majanga ya moto, mafuriko na ajali mbalimbali, hivyo ni vyema ukawa na bima ili unapopatwa na majanga usipate hasara na kuepuka kuyumba kiuchumi. Njoo ukate bima kwa ajili yako na mali zako. NMB inashirikiana na kampuni mbalimbali za utoaji bima”,amesema Urio.

Pia Urio amewakaribisha wananchi na wateja wa Benki ya NMB kutembelea na kufika katika Matawi ya benki ya NMB yaliyopo Karibu na maeneo yao ili waweze kuunganishwa na huduma ya bima inayo unganishwa kwa bei nafuu.

Post a Comment

0 Comments