6/recent/ticker-posts

MHE.KATAMBI AFANYA ZIARA SHINYANGA MJINI NA IBADAKULI ,AELEZA MIRADI YA MABILIONI YA FEDHA ALIYOLETA KWA MAENDELEO SHINYANGA , AMSHUKURU RAIS SAMIA


Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe.Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, akiwa kwenye ziara ya kueleza utekelezaji wa Ilani ya Chama  Mapinduzi (CCM)  chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM ngazi ya kata ambapo amekutana na wajumbe wakata 9 ambazo ni Kata za Kolandoto, lbadakuli, chamaguha,Mjini, Kizumbi, Kitangil, lbinzamata, Ngokoro na  Ndembezi.

Na Amoj media Shinyanga.
MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe.Patrobas Katambi, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha nyingi Jimbo la Shinyanga Mjini na Mkoa kwa ujumla ambazo zimetekeleza miradi mingi ya maendeleo kwa wananchi.

Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, amebainisha hayo leo Julai 11,2024 wakati wa ziara yake ya kukutana na viongozi wa chama cha Mapinduzi ambao ni wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM ngazi ya kata katika kata ya Ibadakuli pamoja na kata ya Shinyanga mjini kwa lengo la kuelezea miaka 4 ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. 

Amesema Rais Samia amefanya mambo makubwa ndani ya uongozi wake wa miaka minne, na ametoa fedha nyingi za maendeleo kwa wananchi ikiwamo na Shinyanga, hivyo hana budi kuendelea kupongezwa juu ya utendaji wake kazi.

"Rais Samia Suluhu Hassan tumpongeze wana Shinyanga ametoa fedha nyingi za maendeleo na mji wetu mnaona umebadilika, miradi ambayo ilikuwa ni kero kubwa imeshatatuliwa ukiwamo ujenzi wa daraja la Iwelyangula na Uzogole sasa hivi wananchi wanapita bila wasiwasi," amesema Katambi.

Aidha, amesema kwa upande wa Sekta ya Afya miundombinu imeboreshwa, ikiwamo na ukamilishaji wa ujenzi wa Hospitali ya Rufani mkoani Shinyanga, na sasa inafanya kazi na kutoa matibabu kwa wananchi pia ametoa Magali 2 ya kubebea wagonjwa katika kituo cha Afya Kambarage pamoja na magari mengine yakubeba wagonjwa katika Hospitali ya Rufani mkoani Shinyanga.


Amesema pia Rais Samia ametoa fedha kwa ajili ya kuimarisha ujenzi wa miundombinu katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi na kukipandisha hadhi kuwa Chuo Kikuu, huku mchakato ukiendelea wa kukipandisha hadhi pia Chuo cha Afya Kolandoto kiwe nacho Chuo Kikuu.

Ameendelea kueleza kuwa Rais Samia, amekuwa akitoa fedha kwa ajili ya kuwainua wananchi kiuchumi, ikiwamo utoaji wa fedha za mikopo kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Amesema pia Rais Samia, ameendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi Barabara kwa kiwango cha Lami, Masoko na Stendi za Mabasi pamoja na utekelezaji wa miradi ya maji safi na salama kwa wananchi.

Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Anod Makombe , amempongeza Rais Samia pamoja na Mbunge Patrobas Katambi kwa kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo. 
 
Aidha amewataka wananchi kupuuza maeneo ya upotoshaji ambayo yamekuwa yakizushwa kuwa miradi ya kimkakati ilivyoanzishwa awamu ya Tano imekwama na kubainisha kuwa miradi hiyo inaendelea kutekelezwa ikiwamo ujenzi wa Reli ya kisasa.


TAZAMA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI



































Post a Comment

0 Comments